Alhamisi, 18 Ramadan 1445 | 2024/03/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Urusi Inakuwa Himaya kwa Mara Nyengine Tena

(Imetafsiriwa)

Mnamo miaka ya 90 ya karne ya 20, wakati serikali kuu ya Urusi ilipokuwa dhaifu, kwa ajili ya kuihifadhi serikali hiyo, ilitengeneza maridhiano mengi na umma na viongozi wa nchi za “jamhuri” na “tawala huru”, kwa ukarimu “kuzifadhili” kwa “mamlaka” bandia ili kuhifadhi nguvu zake juu yao. Aidha, kuvunjika kwa Umoja wa Kisovieti (USSR) kulitokea siku moja kabla, na nchi iligawika na kuwa mataifa 15 huru. Ambapo pia kulibuniwa rasmi kile kinachoitwa CIS – umoja wa mataifa huru ili kubakisha angalau ushawishi kwa baadhi ya mataifa yaliyojitenga na USSR.

Juu ya wimbi hili la kusambaratika kwa himaya ya Kisovieti, watu wa Urusi, ambao ni sehemu ya inayoitwa RSFSR wakati wa Umoja wa Kisovieti, pia zilitaka uhuru. Ili kwa kiasi fulani kuihifadhi RSFSR kutokana na kusambaratika kabisa (ambayo baada ya 1991 ilikuwa ikiitwa Shirikisho la Urusi, na kuwa taifa huru lililojitenga), Moscow (Urusi) iliipatia vyote, “mamlaka” na “jamhuri” katika Urusi “kiasi chochote cha mamlaka iliyoweza kuyachukua”. Hii bila shaka, ilikuwa ni kiini macho na kimsingi ni kuwa kiasi chochote cha “mamlaka” na ”uhuru” uliokuwepo, vyote hivyo havikuwa na utaifa wa kujitenga, bali vilikuwa ni sehemu ya dola moja – Urusi. Na upokonyaji wa yote haya ya “uhuru”, “nafasi maalum”, ni suala la muda tu, na kutegemea tu juu ya nguvu na uwezo wa mamlaka kuu. Wakati huo, ilikuwa ni rahisi kuwazuga watu na wanaharakati na viongozi wa harakati za kitaifa wanaohangaikia uhuru na kujitenga kwa ahadi ya aina kadhaa za maslahi, “uhuru”, hadhi ya “uraisi wa jamhuri”, na kuruhusu uanzishwaji wa Katiba za kieneo, mabaraza ya kutunga sheria, mahakama, na kwa hiyo kuwazuia kutokana na hitajio la uhuru kamili, kujitenga na kuunda serikali huru iliyojitenga. Hata hivyo, vyenginevyo maeneo yote ya Waislamu yangemeguka kutoka Urusi – Tatarstan, Bashkortostan, Chechnya, Dagestan, Ingushetia, Karachay-Cherkessia, Kabardino-Balkaria, Adygea, na kwa usahihi kabisa yangeweza kufuatiwa na Waislamu wote ambao maeneo yao yameishia katika ile inayoitwa mikoa ya “Urusi”, inayokaliwa na watu wa Urusi wasio wa asili baada ya uvamizi – maeneo ya Chelyabinsk, Sverdlovsk, Orenburg, Saratov, Krasnodar nk.

Ikawa kila ambapo Moscow imekuwa na nguvu zaidi, serikali kuu pia ikawa ni yenye nguvu, kidogo kidogo ikawaweka watu watiifu kwa serikali kwenye maeneo nyeti katika “maeneo huru”, au kuwahonga kwa aina tafauti ya marupurupu, kuwapatia fursa “kuimega” bajeti ya ndani, kuwasaliti kwa njia tafauti, kustawi, ambapo hufanywa wajitegemee wenyewe, Moscow ilianza kidogo kidogo kuchukua “maeneo huru” yote haya kutoka kwao, huku ikiwalazimisha kuuza “uhuru”, kwa kubadilishana na viti vyao na nafasi na fursa ya kuwa kwenye beseni la bajeti za ndani na kuwapora watu wao. Yote hayo hapo juu yanatumika Bashkortostan na Tatarstan.

Ni muhimu kutambua kuwa katika miaka ya 90, Waislamu wote walikuwa na fursa ya wazi ya kutoka kwenye ukoloni wa Moscow, kujitenga kabisa na Urusi. Lakini fursa ilipotea, na hisia za kitaifa zilipofifia, kutokana na watu kuvunjika moyo katika harakati za kitaifa, huku kukiwa na kuongezeka kwa propaganda kubwa ya waungaji mkono wa Urusi katika vyombo vya habari na wanasiasa huru na wanahabari kuzimwa na kuenguliwa, Moscow ilianza kuinyima Bashkortostan na Tatarstan maslahi yote hayo na hadhi, “maeneo huru” na “mamlaka kamili”. Benki za taifa na posta zilifilisiwa, sheria za “jamhuri" ziliwekwa sawa kabisa, kuzipelekea kuwa na uwiyano kamili na sheria za Shirikisho la Urusi, kisha Moscow ilianza kuamua sehemu ipi ya bajeti “jamhuri” hizi zitaweka na sehemu ipi itaipatia Moscow.

Sera ikawa ni ya kihimaya zaidi: kwa uondoaji hata wa kimapambo, lakini pia hata alama za mamlaka kamili ya kubuni yalianza: magavana katika kile kinachoitwa “jamhuri” walinyimwa hadhi ya “uraisi”, wa mwisho wao kiongozi wa Tatarstan amenyimwa hadhi hii katika kipindi hichi. Walianza kuitwa “kiongozi wa jamhuri”. Suala la kuitwa tena “jamhuri” katika jimbo lilianza kuzingatiwa, kama lilivyokuwa katika zama za Himaya ya Urusi, wakati utawala wa kijeshi ukiongozwa na gavana mkuu alipotawala katika maeneo yaliyotekwa. Kwa kipindi kirefu, wajumbe wa Raisi wa Shirikisho la Urusi walifanya kazi katika maeneo ya makaazi sambamba na viongozi wa majimbo, maeneo na mamlaka. Kama kabla ya hapo viongozi wa “jamhuri” walikuwa “wakichaguliwa”, au kuteuliwa wawakilishi wa taifa lisilokuwa na mamlaka halisi ya “jamhuri” hizi, hivi sasa Moscow haisiti kuwachagua Warusi kwenye nafasi hizi. Hivi sasa lugha ya jamhuri ya kitaifa imekuwa ikiendelea kusita kuwa “ya kinchi”. Kufundishwa kwake katika shule za serikali kumekuwa sio lazima, na sio zaidi ya masaa 2 kwa wiki. Hivyo, kumekuwa na “kukaza nati” kunakoendelezwa, nguvu kutokea juu inaimarishwa.

Karibuni, udanganyifu huu kwa kinachodaiwa kuwa ni mamlaka umekuwa dhahiri na wazi zaidi, na baadhi ya wamaizi wa mambo wameliweka wazi hili. Kwa mfano, muanzilishi wa chama cha Tatar cha uhuru wa kitaifa “Ittifak” Fauzia Bayramova amepinga hoja ya kwamba Tatar ina dola yake yenyewe. “Hii sio dola, bali utawala wa kikoloni,” alisema mnamo 2019 katika tukio la kumbukumbu. Alitambua kuwa “mamlaka” yote haya ni uwongo na alitaka uondowaji wa ukoloni kwa Watatar. Kwa bahati mbaya, uoni wa wamaizi wa taifa la Tatar umechelewa sana.

Hivi leo, kiwango cha mbinyo dhidi ya Waislamu katika eneo hilo umefikia kilele ndani ya miaka 30 iliopita. Moscow inafuata sera yenye lengo maalum la kuiandika tena historia, kuonyesha uvamizi wake katika sura nzuri, kubaki kimya au kuficha sura ya vurugu la Ubatizaji kwenye Ukristo, na baadhi ya wakati ukweli wa wazi wa ukoloni, kufuta mabaki yote ya historia. Taarifa za kihistoria zinazofichua masimulizi ya kweli juu ya haya zinatambuliwa na mahakama kuwa ni “siasa kali” na zinakatazwa. Hili linathibitishwa na kufungiwa kwa kitabu cha Vakhit Imamov “Historia Iliyofichwa ya Tatar”. Kutekwa kwa Kazan kunaonyeshwa kuwa ni “kuhifadhi na kujilinda”, na siku ya kuanguka kwa Kazan kunaitwa “siku ya kuwaunganisha watu”, na Ivan the Terrible, anachukuliwa kuwa ni mwenye kupongezwa kwa kazi na elimu aliyoipeleka kwa Kazan Khanate na ardhi nyengine za Himaya ijayo ya Urusi. Haya, kwa mfano, tayari ni maoni ya waumini wa kanisa la Kazan.

Katika Bashkortostan, mnamo Oktoba 2021, mchezo wa “The Tale of Kisyabika” ulifutwa ghafla na kuzuiliwa kuonyeshwa. Uigizaji huu unaelezea kisa cha kweli cha mwanamke wa Kiislamu wa Bashkir Kisyabika Bayrasova, aliyelazimishwa kuwa mkristo na kupelekwa kwa wajakazi katika Yekaterinburg. Alikimbia mara tatu kurudi Bashkiria na kurudi kwenye Uislamu, lakini alisakwa na kurudishwa tena. Hatimaye, generali wa Urusi Simonov akaamrishwa auliwe - akiwa mwanamke wa umri wa miaka 60 - kwa kuchomwa, kwa kauli inayojulisha kwenye hukumu ya Februari 8, 1739, kuwa “ameacha Sheria ya Kikristo na kuwa Muislamu.” Mauwaji yalifanyika katika uwanja mkuu wa Yakaterinburg. Hivyo, historia ya kuwaritadisha kwa nguvu Wabashkir chini ya ukaliaji wa kinguvu wa Urusi ilifutwa.

Kwa muda mrefu na bila ya kisingizio chochote, taasisi za Kiislamu na hata mabaraza ya misikiti yalio chini ya mashekhe rasmi zimefilisiwa, bila kutaja ukandamizaji jumla dhidi ya taasisi za Kiislamu ambazo hazipo chini ya wahudumu rasmi. Hii ni kuwa, kama kile kiitwacho “Uislamu wa kidesturi” ulikuzwa dhidi ya uitwao “wa siasa kali”, lakini sasa, baada ya karibu ufilisi kamili au kukamatwa kwa waitwao Waislamu “wenye msimamo mkali”, zamu imekuwa kwa waitwao Waislamu “wenye msimamo wa wastani”.

Kwa kufupisha yote ya hapo juu, ni muhimu kutilia mkazo kuwa muelekeo wa sera kwa Waislamu umebadilika: ikiwa mwanzoni sera hii ni kuwagawa Waislamu kwenye “Waislamu wa kidesturi” na  “wenye siasa kali”, kuwatenga au kuwafunga magerezani wenye siasa kali, na watawala kuhitajia kuwategemea mashekhe rasmi, ili wahalalishe ukandamizaji huu na kuwapa matumaini Waislamu. Hivi sasa, wakati eneo lote “limesafishwa” kutokana na wenye siasa kali, na Waislamu wakiwa wenye hofu, vikosi vya usalama tayari vinaweza kufanya ukatili na ujeuri, bila hata kuficha msimamo wao kwa Uislamu. Watawala hawatosita hadi kusiwepo chochote cha Kiislamu kwa Waislamu, hadi wasimilishwe kabisa. Hali tayari imeshazigeukia lugha za watu wa Tatar na Bashkir, bila kutaja utamaduni, maadili na dini ya watu hawa Waislamu.  Wakati huo huo, wakala wa watawala katika kuwadhibiti Waislamu katika maimam, wahadhiri wa vyuo vikuu vya dini na wanasayansi hawatosimama kando, wale wanaoshirikiana na vikosi maalum watahitaji kujipendekeza hata zaidi, kwa sababu hawawezi kwenda kinyume, kwa kuwa wanategemea watawala katika shughuli zao, na sio kwa Waislamu.

Hali hii ni somo jengine kwa Waislamu, ambao lazima wafahamu kuwa kila wanapojitenga na maagizo ya Uislamu, kuonyesha udhalili au kutafuta mapatano na wavamizi, wataishia kushindwa tu. Jambo muhimu zaidi hivi sasa kwa watu wa eneo hili katika hali za kutowezekana kujivua kutokana na mkoloni ni kutambua hali yao ya kukoloniwa, kusimamisha mashirikiano yoyote na wavamizi na kuwa pamoja katika kurejesha na kuhifadhi kitu muhimu zaidi – dini na maisha kwa mujibu wa sheria zake. Shukrani kwa Mwenyezi Mungu (swt), katika miaka ya karibuni tunaweza kuona miongoni mwa Waislamu wote waliokaliwa na Urusi muelekeo wa muamko wa hisia za dini na siasa, na kila ambapo wakoloni wa Urusi wakijaribu kuzima wimbi hili, muamko wao huwa mkubwa zaidi.

Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema katika Quran:

(إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا يُنفِقُونَ أَمْوَالَهُمْ لِيَصُدُّوا عَن سَبِيلِ اللَّهِ فَسَيُنفِقُونَهَا ثُمَّ تَكُونُ عَلَيْهِمْ حَسْرَةً ثُمَّ يُغْلَبُونَ وَالَّذِينَ كَفَرُوا إِلَى جَهَنَّمَ يُحْشَرُونَ)

“Hakika wale waliokufuru hutoa mali yao ili kuzuilia Njia ya Mwenyezi Mungu. Basi watayatoa, kisha yatakuwa juu yao majuto, na kisha watashindwa. Na wale waliokufuru watakusanywa kwenye Jahannam.” [8:36]

 Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Shaikhetdin Abdullah

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu