Logo
Chapisha ukurasa huu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Kuhasiwa kwa Nguvu Wanawake wa Kiislamu wa Uighur Kumethibitishwa na Ushuhuda wa Moja kwa Moja

Mnamo tarehe 4 Septemba 2020 gazeti la The Guardian limeripoti juu ya ushuhuda wa mwalimu Muislamu wa Kiuighur aliyelazimishwa kufanyiwa hatua nyingi za kudhibiti kizazi baada ya kupata vitisho vya mara kwa mara kwa maisha yake na ya familia yake.

Qelbinur Sidiq mwenye miaka 50 alizingatiwa kuwa ni Muislam “mwenye msimamo wa wastani” aliyefanya kazi katika shule za serikali za China na alikuwa ametii sera ya mtoto mmoja. Alikuwa amejitolea kibinafsi kutokuwa na watoto na alikuwa ameshapita umri wa kawaida wa kuzaa. Hata hivyo, alipokea maagizo ya ujumbe wa maandishi uliomtishia yeye na familia yake kama hatokubali kuwekewa chombo cha IUD. Jumbe za maandishi zilionyeshwa kwa wanahabari kama ushahidi na zinasomeka; “Iwapo chochote kitatokea, nani atawajibika kwako? Usibahatishe kuhusu maisha yako, hata usijaribu. Mambo haya hayapo kukuhusu wewe. Lazima ufikirie kusuhu watu wa familia yako na jamaa zako waliokuzunguka… Kama utapambana nasi mlangoni kwako na ukakataa kushirikiana nasi, utapelekwa kituo cha polisi na kukaa juu ya kiti cha chuma!”

Kwa kuhofia maisha yake na familia yake, alikubali kuwekewa vifaa hivyo bila hiari yake lakini alitoa pesa ili kutolewa “kinyume na sheria” baada ya kuhisi matatizo makubwa ya kiafya. Katika uchunguzi wa kawaida maafisa wa ndani wamegundua na kuamriwa kuwekewa vifaa vyengine vipya. Hatimaye matibabu yake yaliishia kuhasiwa kizazi. Alielezea kuwa huu ni utaratibu mpya wa kawaida kwa wanawake wote wa Uighur walio kati ya miaka18 hadi 59.

Kitengo cha Wanawake cha Afisi Kuu ya Hizb ut Tahrir kimeripotia juu ya mateso kwa Waislamu wema kwa miaka mingi nchini China. Tumefichua kambi za mateso ambapo wanaume, wanawake na watoto wamepotea na wamezuiliwa kinyume na matakwa yao, na mara nyingi wamekuwa wakiteswa.

Hatusubiri wasaliti wa serikali katika ulimwengu wa Wamagharibi na wa Kiislamu kuzungumza kwa niaba ya wahanga hawa wasio na hatia. Tunajua kuwa maslahi ya kifedha na kiutawala huja mwanzo kabla ya sera zao bandia za haki za binaadamu. Viongozi wetu wenyewe Waislamu hawana uhuru wa kuwaokoa dada zetu kwa kuwa hulka zao za uoga zinatumikia kulinda nafasi zao haramu wakiwa ni watawala vibaraka katika ardhi zetu. Tuna imani tu katika sauti ya ukweli iliounganishwa na matendo ya Ummah wetu kote ulimwenguni kufichua maovu haya ya aibu dhidi ya kina mama wetu na kufichua mateso yasiyovumilika kwenye kila jukwaa la habari linalopatikana. Tunatoa wito kwa ndugu zetu na dada zetu kila mahala kufanya haya pamoja kwa kuunga mkono kurejea kwa Khilafah kwa njia ya Mtume (saw) ili dada zetu wote ulimwenguni waweze kukombolewa kutokana na dhulma za aina zote.

Mwenyezi Mungu (swt) anasema katika Quran kwamba kuwa Muislamu ni uovu tosha kwa wengi na kisa cha dada yetu Quelbinur ni mfano wa hayo;

وَلَن تَرْضَى عَنكَ الْيَهُودُ وَلاَ النَّصَارَى حَتَّى تَتَّبِعَ مِلَّتَهُمْ قُلْ إِنَّ هُدَى اللّهِ هُوَ الْهُدَى وَلَئِنِ اتَّبَعْتَ أَهْوَاءهُم بَعْدَ الَّذِي جَاءكَ مِنَ الْعِلْمِ مَا لَكَ مِنَ اللّهِ مِن وَلِيٍّ وَلاَ نَصِيرٍ﴿

“Mayahudi hawawi radhi nawe, wala Wakristo, mpaka ufuate mila yao. Sema: Hakika uongofu wa Mwenyezi Mungu ndio uongofu. Na kama ukifuata matamanio yao baada ya ujuzi uliokwishakujia, hutapata mlinzi wala msaidizi kwa Mwenyezi Mungu.” [2-120]

Kufahamu uongofu wa Muumba wetu, Mwenyezi Mungu (swt) ndio njia sahihi pekee ya kutuwezesha kama wanawake na ni kwa Khilafah pekee ndipo tunaweza kuiona salama na amani kwa haki zetu zote kama Ummah mmoja katika ulimwengu, pamoja na kuangaliwa wanaadamu wote kama alivyoamrisha Mwenyezi Mungu (swt).

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Imrana Mohammed

Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.