Ijumaa, 10 Shawwal 1445 | 2024/04/19
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Kuunganishwa kwa Nguvu Kashmir Iliokaliwa Kimabavu: ni Mshtuko wa Kuchochea Uhuru wa Kweli Kutokana na Ukoloni

Agosti 5, mwaka 2020 ilitimiza mwaka mmoja tokea Modi (Raisi wa India) alipoanza mzingiro kwa Kashmir iliokaliwa kimabavu. Sasa tumeingia mwaka wa pili wa uunganishaji wa nguvu wa Modi, kwa ukandamizaji wa kinyama dhidi ya Waislamu kwenye ardhi ya Kashmir iliotekwa na mashambulizi kadhaa dhidi ya Azad Kashmir (Kashmir iliokombolewa), ili kulitambulisha eneo lake jipya analolidai.

Kwa tukio kama hili baada ya miongo kadhaa ya upinzani wenye msingi wa haki na ari, ulioanzia kabla ya uhuru wa Pakistan Agosti 14 mwaka 1947, limekuwa na mshtuko kwa Waislamu. Mshtuko unajitokeza kwa hisia za kuchanganyikiwa na kukata tamaa, kwa Waislamu wa Pakistan, pamoja na hisia za kusalitiwa na kutelekezwa, kwa Waislamu wa Kashmir. Mshtuko uko mbali na kupungua na umeanza kukusanyika kwenye uoni mmoja wa kisiasa, kupitia mjadala ulioenea na kuhusisha juu ya kwa nini na kwa vipi kutokea majanga haya.

Ni wazi kwetu kuwa azimio muwafaka la Kashmir Iliokaliwa Kimabavu halituepuki kwa sababu ya maslahi ya kimada, ima yawe ya kiuchumi au uwezo wa kijeshi. Linatuepuka kwa sababu ya mtazamo wa kisiasa wa watawala wa sasa wa Pakistan. Badala ya kukusanya rasilimali zetu wenyewe ili kuhifadhi haki zetu tulizokoseshwa muda mrefu, uongozi wa sasa unajipeleka kwa mataifa makubwa ya kikoloni ambayo yanaendesha jamii ya kimataifa, kupitia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Hata hivyo, tuzingatie kuwa, hivi leo, uongozi wa Pakistan wenyewe ni tegemezi kwa wakoloni. Utawala wa Bajwa-Imran hauendi sambamba na ummah, ukiamsha dharau zao na lawama kwa misimamo yao na kwa hatua dhaifu ambazo ni matokeo yake. Baada ya hayo yote, msimamo wa utawala unagongana na yote tunayoyaelewa katika Dini yetu na historia yetu. Umoja wa Mataifa mara kwa mara umekuwa ukiwagonga Waislamu katika mambo yao, na hali wakiwa kimya au kuendeleza usaidizi kwa wale wanaofanya dhulma kwa Waislamu, ima ikiwa katika Srebrenica miaka ishirini na tano iliopita, au Kashmir Iliokaliwa Kimabavu hivi leo. Zaidi ya hayo, kusubiria kwetu uhuru kutoka kwa dola za makafiri hakujazalikana na hisia za mapenzi ya zama za utawala wa Kiislamu. Kusubiria kwetu kunachipuza kutokana na Imani isioyumba ya Uislamu wenyewe, kupitia ufahamu wa misingi ya nguzo za uendeshaji wa dola na mahusiano ya kimataifa yenye kuonyeshwa katika Sunnah za Mtume (saw) na kuigizwa na Makhalifa Waongofu (ra).

Kimsingi ni tofauti na hisia na fikra zetu, kipote cha sasa cha wanasiasa na jeshi hakiwezi kutuongoza. Ni mabaki yanayoendelea ya zama za wakoloni zilizoanza kuota mizizi yake katika Bara Hindi mwaka 1657, kabla ya kuangushwa kwa Khilafah mwaka 1924. Ni kipote hiki ndicho kilicho kuzwa na mkoloni mwenyewe, kulishwa sumu ya maadili ya Wamagharibi, tabia, fikra na mtindo wa maisha. Kipote hiki kimeanzishwa juu ya vichwa vyetu kupitia kupatiwa nafasi katika Serikali ya Kifalme na Jeshi la Uingereza. Hata baada ya uhuru, mazingira ya sasa ya kisiasa na kijeshi yamechafuliwa kwa sumu ya mkoloni. Kutojiamini kumekuwepo kwa vipote vyote vya wanasiasa na jeshi, kwa Imani kuwa sisi si chochote bila usaidizi wa wakoloni.

Ni wazi kuwa, chini ya uongozi wa sasa, hatutojua kabisa uhuru kutoka kwa wale wanaotudhuru na kuwasaidia wengine katika kutudhuru. Mshtuko mbaya wa kupoteza Kashmir Iliokaliwa Kimabavu lazima utuchochee kusimamia mambo yetu kwa sheria za Dini yetu. Ni pale tu tutaposimamisha hukumu kwa yale yote aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu (swt), ndipo tutatawaliwa na uongozi mpya, walinganizi wa sasa wa Khilafah. Ni wakati huo tu ndipo tutapoonja mwamko ambao tumeuepuka kwa muda mrefu sana, na hivyo kuweza kudai haki zetu, ima ni ardhi Iliokaliwa Kimabavu ya Kashmir au nafasi yetu Ummah bora ulioletwa kwa watu. 

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Musab Umair - Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu