Ijumaa, 19 Ramadan 1445 | 2024/03/29
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Imran Khan Anashirikiana na Mtesaji wa Waislamu: Udikteta wa Kichina Unaopinga Uislamu juu ya Waislamu wa Uyghur wanaokandamizwa

 (Imetafsiriwa)

Mnamo siku ya Alhamisi Julai 1, Waziri Mkuu wa Pakistan Imran Khan aliwathibitishia wanachama wa vyombo vya habari vya China msaada wake kwa sera za serikali ya China huko Turkestan Mashariki. Alisema kuwa kwa sababu ya "uhusiano imara sana wa Pakistan pamoja na Cihina", anaamini sura ya Beijing ya muamala wake kwa Waislamu wa Uyghur juu ya ushahidi mkubwa kutoka kwa mashirika ya haki za binadamu, wataalamu na ushuhuda wa eneo hilo kutoka kwa Waislamu wa Uyghur wa ukatili na ukandamizaji ambao Waislamu wameteseka nao eneo la 'Xinjiang' mikononi mwa udikteta wa China. Khan pia aliusifu mfumo wa kisiasa wa China, akisema kwamba sheria ya Chama chake cha Kikomunisti ilitoa badali na mfano bora wa utawala kwa mfumo wa kidemokrasia. Juni hii, katika mahojiano na wavuti wa habari wa Amerika Axios, Waziri Mkuu Khan alikataa kulaani au hata kutambua ukandamizaji wa China kwa Waislamu wa Uyghur huko Turkestan Mashariki. Alipoulizwa na mwenye kuhoji ni kwa nini alikuwa kimya juu ya suala hilo, alijibu kwamba alikuwa akizingatia matukio ndani ya taifa lake na mpakani. Alikumbushwa mara moja na mwandishi huyo wa habari kwamba mateso ya Waislamu wa Uyghur yalikuwa yakitokea katika mpaka wake.

Imran Khan, kama ilivyo kwa watawala wote wasaliti wa nchi za Waislamu, ameuza roho yake kwa mzabuni wa hali ya juu. Haoni chochote isipokuwa dolari zinazohusiana na biashara zake na China, haswa dolari bilioni 60 ambazo China imewekeza nchini Pakistan katika miradi ya Ukanda wa Uchumi wa China na Pakistan ya mpango wake wa Ukanda na Barabara. Kwa ajili ya pato la kimada, Khan anachagua kupuuza kwa khiari mauaji ya halaiki ya kidini ya China dhidi ya Waislamu wa Uyghur yenye lengo la kufuta kitambulisho chao cha Kiisilamu na uwepo wa Uislamu Turkestan Mashariki kupitia ufuatiliaji mkubwa wa idadi ya Waislamu, mbinu za kuwatishia, kupotezwa kimabavu na kuwekwa kizuizini kwa wingi. Kulingana na Ripoti ya Haki za Binadamu, "Vunja Ukoo wao, Vunja Mizizi yao", tangu 2017, ukamatwaji huko Turkestan Mashariki ni asilimia 21 ya watu wote waliokamatwa nchini China licha ya eneo hilo kuwa na  asilimia 1.5 tu ya watu wote. Ripoti hiyo pia ilisema kuwa ukamatwaji katika eneo hilo uliongezeka kwa asilimia 306 katika miaka 5 iliyopita. Tangu 2017, serikali hiyo pia imeharibu au kubomoa theluthi mbili ya misikiti katika eneo hilo. Fauka ya hayo, Mei hii, Mradi wa Haki za Binadamu wa Uyghur ulitoa ripoti yake, "Uislamu Umetwaliwa: Unyanyasaji wa China wa Maimamu wa Uyghur na Watu Mashuhuri wa Kidini" ambayo ilisema kwamba zaidi ya maimamu 1000 wa asili ya Kiturkic wamewekwa kizuizini huko Turkestan Mashariki na kutaja Pakistan kuwa miongoni mwa nchi ambazo zimeisaidia China kuwakamata maimamu katika eneo hilo. Wengi wa walizuiliwa kwa kuswali tu swala za jamaa au kuhubiri Uislamu.

Kama inavyojulikana sasa, zaidi ya Waislamu milioni 1 wamefungwa katika kambi za mateso katika eneo hilo ambapo wamekumbana na kuritadishwa kwa kulazima kwa imani za kikomunisti za kipagani, kulazimishwa kunywa pombe na kula nyama ya nguruwe, na kufanyishwa kazi ya lazima. Wengi wa wale waliowekwa kizuizini pia wamevumilia mateso makali ya kimwili na kisaikolojia, huku wanawake wa Kiislamu wa Uyghur wakikumbwa na ubakaji wa kimpangilio, ufungwaji kizazi wa lazima na uavyaji mimba. Wakati huo huo, watoto wa Waislamu hao waliowekwa kizuizini wametenganishwa na familia zao na kuwekwa katika vituo vya watoto yatima vinavyoendeshwa na serikali ambapo pia wanachafuliwa mabongo yao kuachana na Uislamu. Sambamba na hayo, serikali ya Kichina imetekeleza sera ya kudhibiti uzazi kwa Waislamu wa Uyghur na Waislamu wengine walio wachache huko Turkestan Mashariki. Kulingana na ripoti moja iliyochapishwa Juni hii na Adrian Zenz, mtafiti wa shirika lisilo la kujipatia faida, "Waathiriwa wa Wakfu wa Ukumbusho wa Ukomunisti" Sera za Beijing za kutekelezwa kwa mipaka ya uzazi, uhamishaji wa wafanyikazi wengi hadi maeneo mengine na kufungwa kwa Waislamu wengi kwa muda mrefu kutapunguza hadi uzazi Milioni 4.5 wa Uyghurs na Waislamu wengine walio wachache katika eneo hilo ndani ya miaka 20. Kiwango cha uzazi tayari kimepungua kwa karibu asilimia 50 kati ya 2017 na 2019 katika eneo hilo. Haishangazi kwa hivyo, mamlaka za China zimetuhumiwa na mashirika ya kutetea haki za binadamu kwa kutekeleza uhalifu dhidi ya wanadamu na kuunda "eneo la kuzimu kwa kiwango kikubwa" dhidi ya Waislamu huko Turkestan Mashariki.

Imran Khan daima amejionyesha kama bingwa wa Uislamu na kiongozi mwanakruseda dhidi ya hofu ya Uislamu. Mwaka jana, alitoa hotuba kali kwa Umoja wa Mataifa akionya kuongezeka kwa hofu ya Uislamu ulimwenguni. Lakini, kupuuzia kwake mateso makali ya Waislamu wa Uyghur ili kujipendekeza kwa marafiki wake wa Kikomunisti wa China inaonyesha mara nyengine tena jinsi alivyotumia kadi ya "Uislamu" kujaribu kushinda uungwaji mkono mkubwa na uchaguzi. Anasema kuwa amezingatia tu matukio ndani ya taifa lake mwenyewe. Tunauliza: je, taifa lake sio Ummah wa Rasulillah (saw)? Je! Waislamu wa Uyghur sio sehemu ya Umma huu wa Uislamu? Je! Mwenyezi Mungu (swt) hasemi kuwa:

 (إِنَّ هَذِهِ أُمَّتُكُمْ أُمَّةً وَاحِدَةً وَأَنَا رَبُّكُمْ فَاعْبُدُونِ) “Indeed! This Ummah is one Ummah, and I am your Lord so worship Me (alone).” [Al-Anbiyaa: 92]? Fauka ya hayo, Khan anadai kwamba anaunga mkono muundo wa utawala wa Madina, huku wakati huo huo akisifu mfumo wa kisiasa wa kidikteta wa kikomunisti ambao unamkataa Mwenyezi Mungu (swt) na unaupiga vita Uislamu! Yote haya yanaonyesha kwamba Waziri Mkuu Imran Khan amekatwa kutoka kitambaa hicho hicho kilichooza kama watawala wa zamani wa kisekula 'Ruwaibidhah' ambao walionyesha kupuuza kabisa Uislamu na sheria zake.

Mtume (saw) amesema:

«سَيَأْتِي عَلَى النَّاسِ سَنَوَاتٌ خَدَّاعَاتُ يُصَدَّقُ فِيهَا الْكَاذِبُ وَيُكَذَّبُ فِيهَا الصَّادِقُ وَيُؤْتَمَنُ فِيهَا الْخَائِنُ وَيُخَوَّنُ فِيهَا الْأَمِينُ وَيَنْطِقُ فِيهَا الرُّوَيْبِضَةُ قِيلَ وَمَا الرُّوَيْبِضَةُ قَالَ الرَّجُلُ التَّافِهُ فِي أَمْرِ الْعَامَّةِ»

“Itawajia watu miaka ya udanganyifu, mrongo atasadikiwa na mkweli atakadhibishwa, khaini ataaminiwa na mwaminifu atakhiniwa; na Ruwaibidha ndio watakaotamka maamuzi.' Mtume (saw) akaulizwa: 'Ruwaibidha ni nani?' Mtume (saw) akasema" 'Mtu asiye na kima wala maadili katika mambo ya watu.”

Iliwatosha kwa watawala hawa Ruwaibidha! Umetosha uwongo wao na kushirikiana na maadui wa Uislamu! Imetosha kucheza kwao na hisia na matumaini ya Kiislamu ya Umma huu! Umma huu unastahili na unatamani uongozi ambao utaakisi imani zao nzito za Kiislamu, na utailinda Dini yao na kaka na dada zao kote ulimwenguni. Hakuna mwengine isipokuwa Khilafah kwa njia ya Utume ndio utakaotoa uongozi kama huo. Hivyo basi imetosha kuwarudisha rudisha watawala wa Ruwaibidha! Hebu na tuweke mkazo na juhudi zetu zote katika kusimamisha Mfumo wa Mwenyezi Mungu (swt), Khilafah ambayo peke yake inastahili utiifu na uungaji mkono wa Waislamu.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Dkt. Nazreen Nawaz
Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu