Ijumaa, 19 Ramadan 1445 | 2024/03/29
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon

H.  2 Ramadan 1441 Na: H.T.L 1441/07
M.  Jumamosi, 25 Aprili 2020

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Mamlaka Inayoipa kipaumbele Kamari (na Aina zake) juu ya Ibada ya Mwenyezi Mungu!!!
(Imetafsiriwa)

Janga la virusi vya Korona limeutingisha ulimwengu, kusitisha shughuli zake na kuwaacha wanasiasa wake katika mshangao na mashaka. Chumi ambazo zilikuwa zikidai kuwa zenye nguvu zaidi zinaporomoka, na nidhamu za afya zimeharibiwa katika nchini zinazojiita zilizoendelea. Wakati virusi vya Korona vilipoingia Lebanon, uzembe ulionekana dhahiri kutoka kwa serikali, kwa mzozo wa kisiasa, kama ilivyo kuwa kwa kuruhusu kuingia kwa ndege kutoka kwa maeneo yaliyoathirika.

Ulimwengu ulipoarifiwa na kufungwa kwa mipaka na ndege, Lebanon ikafuata nyuma yao kama kawaida bila mwongozo, na kufunga njia zote za maisha, katika nchi ambayo watu wake wengi wanaishi kwa kazi za siku hadi siku ili kupata chakula chao cha kila siku.

Wakati Mamufti wa Al-Azhar na Hijaz walitaka kufungwa kwa Al-Azhar na Al-Haramain (Makkah na Madina), Mamufti wa Lebanon walitoa wito wa kufungwa kwa misikiti, na hatukusikia utafiti wa kina wa kifiqhi, lakini badala yake waliwafuata wale waliofuata njia hii, pia bila mwongozo, hata bila uthibitisho wa wazi. Katika hali hii, tunawaalikeni kusoma yale ambayo Amiri wa Hizb ut Tahrir, mwanachuoni mkubwa Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah, ametoa kuhusu uhalisia wa virusi vya Korona, na kusoma majibu yake ya maswali juu ya hukmu za kufunga misikiti, na kuhusu njia ya kisheria ya kukabiliana na majanga na maambukizi.

Hatukupenda kuwahutubia mamufti kwa hili, tukisema: ugomvi wetu nao sio suala hili, na tunatoa udhuru kwa hofu yao iliyozidi, katika nchi ambayo wanasiasa wake wa ubaguzi wa rangi wanangojea fursa yoyote kushambulia bali kukandamiza Uislamu na watu wake, lakini kwa jambo hili kutangazwa kwa hatua za kuondoa marufuku ya kufungwa, na kufunguliwa kwa sehemu za maovu na kamari kabla ya kufunguliwa kwa misikiti yetu, basi hapana, naapa kwa Mwenyezi Mungu, hili ni janga, na utovu wa nidhamu dhidi ya Dini ya Mwenyezi Mungu na waja wake, ambao nyoyo zao zinaungua kwa maumivu kwa kuzuia Ijumaa yao na swala za jamaa, na wakameza sumu ya kufungiwa katika mwezi wa ibada yao, mwezi uliobarikiwa wa Ramadhan, ili isisemwe maambukizi yalitoka misikitini!

Kwa hivyo, mamlaka dhalili hukutana na ukimya huu na kuridhia licha ya hisia za huzuni leo kwa kutoa hatua za kuhamasisha umma, na kuifanya hatua ya tatu kuwa hatua ya kufunguliwa kwa maeneo kadhaa mnamo 11/5/2020, ikiwemo casino, inayojulikana kama Casino ya Lebanon, na hatua ya nne mnamo 25/5/2020 kufungua shule, vyuo vikuu na vituo vya ununuzi. Ama kwa hatua ya tano, mnamo 8/6/2020, itafungua sehemu kadhaa, pamoja na "sehemu za ibada".

Je! Serikali hii inafuata njia gani katika mipango ya kufungua na kufunga (maeneo)?! Jibu letu halipingiki; inafuata njia ya usekula wake wenye chuki, haswa mkuu wa serikali yake, Hassan Diab. Je! Casino, ambayo itafunguliwa kwa asilimia 70 ya uwezo wake, kama ilivyo ainishwa katika tangazo, na vyuo vikuu, shule na vituo vya ununuzi, vina mikusanyiko midogo kuliko misikiti?! Je, hazikuwa sehemu hizi zilizo funguliwa kwanza, ndio zenye mikusanyiko mikubwa?! Je! haukuwa wakati mrefu zaidi wa kuwasiliana uko katika maeneo kama haya?! Ilhali wakati wa mawasiliano katika misikiti ni mdogo bali ni mchache zaidi, je, ni sehemu ambayo wale tu wanaotawadha na kuoga ndio wanaweza kuingia, na hizi ndizo hatua za kwanza za kujikinga (dhidi ya virusi hivi).

Tunaionya mamlaka kutokana na mbinu hii ya kuudhi, ambayo inachokoza hisia na imani za Waislamu, ambao wamejaribu kufungua misikiti yao katika maeneo kadhaa, kwa hivyo je mamlaka hiyo inafanya kazi au inataka kuwasukuma Waislamu ili kugombana?

Tunawahutubia mamufti kuwa kunyamazia kimya maamuzi haya ni matusi kwa Dini na wafuasi wake na kuwachukia dhidi yao, na hatutakaa kimya kwa hilo, na pia nyinyi hamupaswi kukaa kimya, katika nchi ambayo hatua huchukuliwa pasi na mwelekeo wa kisheria au wa kisayansi, wala hata (kwa kuzingatia) idadi ya visa vya maambukizi, na tuna hakika kabisa na yale ambayo Mtume wetu (saw) amesema:

«الْإِسْلَامِ يَعْلُو وَلَا يُعْلَى عَلَيْهِ»

“Uislamu daima ndio unao olea na hakipaswi kuolea kitu juu yake.”

Kwa hivyo, fikiria jukumu lako kabla ya kupoteza nafasi yako, na utilie maanani maneno ya Mwenyezi Mungu (swt):

[لَّمَسْجِدٌ أُسِّسَ عَلَى التَّقْوَىٰ مِنْ أَوَّلِ يَوْمٍ أَحَقُّ أَن تَقُومَ فِيهِ فِيهِ رِجَالٌ يُحِبُّونَ أَن يَتَطَهَّرُوا وَاللَّهُ يُحِبُّ الْمُطَّهِّرِينَ]

“Msikiti ulio jengwa juu ya msingi wa uchamngu tangu siku ya mwanzo unastahiki zaidi wewe usimame ndani yake. Humo wamo watu wanao penda kujitakasa. Na Mwenyezi mungu anawapenda wanao jitakasa.” [At-Tawba: 108].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Wilayah Lebanon

 #كورونا   #Covid19         #Korona       

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Lebanon
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu