Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  25 Safar 1443 Na: 1443 H / 009
M.  Jumamosi, 02 Oktoba 2021

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Shavkat Mirziyoyev Anamfuata Mwalimu wake wa Kiimla Karimov
katika Kuwatesa Wanawake wa Kiislamu
(Imetafsiriwa)

Mahakama ya Upeo ya Tashkent ilitoa taarifa rasmi juu ya habari zinazozunguka juu ya kukamatwa, kama hatua ya tahadhari, kwa Bi M. M. ambaye alichapisha nyezo zilizoharamishwa kwenye Facebook. Kwa mujibu wa mwandishi wa chapisho hilo, maafisa wa kupambana na ugaidi katika wilaya ya Yunusabad wamemkamata mwanamke huyo kutoka nyumbani kwake na kwa sasa anazuiliwa katika Gereza la Tashturma. Kulingana na chanzo kilichochapishwa kwenye daryo.uz, inashukiwa kuwa M.M. ametenda kosa chini ya kifungu cha 244-1 (kuandaa, au kuhifadhi, au kusambaza au kuonyesha nyenzo zinazotishia usalama wa umma au utangamano wa umma), Kifungu cha 3, Sehemu ya G ya Kanuni ya Jinai. Rustam Bek Karim, mwanabloga, alisema kwenye ukurasa wake wa Facebook kwamba karibu wanawake 56 wanazuiliwa, ambao wote wameshtakiwa chini ya kifungu cha 244 (3) (g) cha Kanuni za Adhabu. Kesi hizi zote za jinai ni za uwongo. Wanawake hao walituhumiwa kwa sababu ya kuhifadhi na kusambaza hotuba za Maimamu kama vile Abdullah Dhaffar na Sadiq Samarkandi kwenye kurasa zao za Facebook. Mamlaka rasmi hazikutoa taarifa rasmi au chochote kuhusu kukamatwa kwao.

Uzbekistan kwa sasa inajiandaa kwa uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika Oktoba 24. Watu wa Uzbekistan hawataki Shavkat Mirziyoyev abakie kama raisi. Kwa hivyo, wataandamana mabarabarani kudai afutwe kazi kwa sababu wakati wa miaka ya utawala wake, hakusuluhisha matatizo ya watu, lakini badala yake maisha yalikuwa magumu kuliko hapo awali, na haki za binadamu zinakiukwa zaidi na zaidi. Watu wamechoshwa na ukosefu wa ajira, umaskini, uonevu, mateso, ufisadi, dhulma na rushwa.

Baada ya miaka mingi ya utawala wa kidikteta wa dhalimu Karimov, watu wa Uzbekistan walimpa ujasiri mkubwa Shavkat Mirziyoyev na walidhani kuwa atawatoa gizani na kuwaingiza kwenye nuru. Lakini, kuchukua kwake mamlaka kulikuwa kama kutumbukia katika dhoruba nzito ili kukimbia mvua! Majina yamebadilika, lakini msingi haujabadilika. Wanawake wa Kiislamu wanaozuiliwa katika Gereza la Tashturma walikuwa wameenda kutafuta ruhusa ya kuwatembelea waume zao gerezani. Matokeo yake, wameshtakiwa kwa kusambaza nyenzo za kidini zilizopigwa marufuku. Hata waandishi wa habari na wanabloga ambao wamekuwa wakishughulikia masaibu ya watu na unyama uliofanywa na serikali wamefungwa gerezani kwa kila aina ya tuhuma za uwongo. Ilifikia hata kulazimisha wanabloga na wanaharakati wa haki za binadamu kuamua kukaa katika hospitali za afya ya akili! Serikali ya Uzbek inaamini kuwa kuwafungia wale wanaolalamikia ukatili katika magereza na hospitali na kunyamazisha sauti zao, kunatoa taswira kuwa matatizo yote yamesuluhishwa, lakini ukweli hauwezi kufichwa kama vile methali maarufu miongoni mwa Wauzbeki, 'Huwezi kuficha mwezi kwa sketi, na ukificha maradhi, homa itayadhihirisha'.

Enyi Wanaume na Wanawake Waislamu nchini Uzbekistan: Serikali haisuluhishi matatizo yenu, bali wale walio na mamlaka hutanguliza maslahi yao ya kibinafsi kwanza, kabla yenu. Wanaupenda uongozi kwa sababu ya kupata utajiri, mitindo ya maisha ya kifahari, na umaarufu, na hawasiti kuwatoa kafara kwa ajili yake. Hawasikilizi malalamiko ya watu, tofauti na Khalifa Omar Al-Faruq, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, ambaye alikuwa akizunguka mjini wakati mwingine kwa kujificha, akificha sura yake ili kuona jinsi raia wake wanavyoishi, isije ikawa kuna wale wanaoona haya kumlalamikia.

Watawala hawa wenu sio kama Omar al-Faruq, kwa hivyo inukeni na mchague kuishi kulingana na Sheria ya Mwenyezi Mungu (swt), kwa sababu ni mfumo wa kimungu na una uwezo wa kumaliza dhulma zote na matatizo yote. Na kisha, hatutawapata wanawake wa Kiislamu katika magereza kama wahalifu, bali tutawakuta majumbani mwao, wakilea watoto wao, wakiwasha kurunzi ya familia.

Msishiriki katika uchaguzi wa urais kutaka rais mpya kuchukua nafasi ya Shavkat Mirziyoyev kwa sababu ikiwa mtu anayetawala kwa sheria zile zile zilizotungwa na wanadamu atakuja mahali pake, hakuna kitakachobadilika. Fauka ya hayo, kusimamishwa kwa Dola ya Khilafah kwa njia ya Utume ni wajibu juu yenu. Mwenyezi Mungu (sw) asema:

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللَّهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَأُولِي الْأَمْرِ مِنكُمْ]

“Enyi mlio amini! Mt'iini Mwenyezi Mungu, na mt'iini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi.” [An-Nisa’: 59].

Utiifu kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake utakuwepo tu chini ya Dola ya Khilafah Rashidah pekee. Leo, tunahitaji dola hii ili tuishi kulingana na sheria za Uislamu. Ama serikali ya kisekula, kama mlivyoshuhudia, haitabikishi sheria ya Mwenyezi Mungu (swt), bali iko dhidi yake na inawapiga vita Waislamu na haioni aibu kuwaua. Kwa njia hii, wanataka kuizima nuru ya Uislamu, lakini nuru ya Uislamu itaenea kote ulimwenguni, Mwenyezi Mungu akipenda.

 [يُرِيدُونَ أَن يُطْفِؤُواْ نُورَ اللّهِ بِأَفْوَاهِهِمْ وَيَأْبَى اللّهُ إِلاَّ أَن يُتِمَّ نُورَهُ وَلَوْ كَرِهَ الْكَافِرُونَ * هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَى وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ وَلَوْ كَرِهَ الْمُشْرِكُونَ]

“Wanataka kuizima Nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao, na Mwenyezi Mungu anakataa ila aitimize Nuru yake ijapo kuwa makafiri watachukia. Yeye ndiye aliye mtuma Mtume wake kwa uwongofu na Dini ya Haki ipate kushinda dini zote, ijapo kuwa washirikina watachukia.” [At-Tawba: 32-33]

 Kitengo cha Wanawake

katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.