Alhamisi, 18 Ramadan 1445 | 2024/03/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kenya

H.  26 Dhu al-Qi'dah 1441 Na: 1441/12
M.  Alhamisi, 16 Julai 2020

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Chini ya kisingizio cha kupambana na COVID-19 kunafanywa bidaa mpya kwa Dini yetu

Serikali kupitia baraza la dini mseto (Inter- Faith) imefungua misikiti kwa mikakati mikali. Jopo hilo la wanachama kumi na tano lilipewa jukumu la kufanyakazi na wizara ya mambo ya ndani pamoja na wizara ya afya katika kuweka masharti ya kufunguliwa tena maabadi. Kati ya masharti hayo yanayopaswa kufuatwa kwenye nyumba za ibada ni; kuweka umbali wa masafa ya mita 1.5 baina wanaoswali, idadi ya watu 100 pekee kuruhusiwa kuabudu, watoto chini ya umri wa miaka 13 na watu wazima wenye umri wa miaka 58 kutoruhusiwa kuingia kufanya ibada na muda wa kufanya ibada usizidi saa moja.

Kwa haya, tungependa kueleza yafuatayo:

Fikra jumla ya maingiliano ya kiimani ni fikra ya kisekula isio na msingi wowote katika Uislamu. Hii ni kuwa fikra hii inatoa mwito wa kuweko na uwiano baina ya imani mbalimbali za Kidini. Fikra hii aidha inalingania dini nyengine mpya kinyume na Uislamu ambayo Wamagharibi wanataka Waislamu wote kote duniani kuikubali dini hiyo. Binafsi wazo hili linalenga kuwafanya Waislamu waachane na mafundisho yao ya Kiislamu badali yake fikra za kisekula iwe ni kipimo cha Dini yao.

Sheria za Kiislamu zimetoka kwa Mwenyezi Mungu SWT (Wahyi), katu hazibadilishwi na mamlaka yoyote yale, tofauti na  kanuni za Kisekula zinazo tokamana na akili za mwanadamu hivyo huwekwa na kubadilishwa kulingana na mazingira. Na ndio kwa muktadha huu, twakumbusha masheikh ambao baadhi yao ni wanajopo wa baraza la Interfaith, walichotakikana ilikuwa ni kuweka bayana sheria za Kiislamu kuwa hazichukuliwi mahala popote pale ila kwenye machimbuko yake asili ambayo ni Quran, Sunna na Ijmaa na Qiyas. Hili ndilo jukumu la wanavyuoni wamchao Mungu nao hupaza kauli ya haki pasina kuogopa lawama ya mwenye kulaumu.

Utekelezwaji wa ibada ya Swala za Jamaa umeonyeshwa kivitendo na Mtume wetu Muhammad (Saw), hivyo si suala la kufanyiwa mashauriano. Kwa hali hii, ni faradhi kwa Waislamu wote kupanga safu wakiwa kwenye swala pasina kuacha mwanya baina ya mtu mmoja na mwengine. Amepokea Almaalik Bin Al-huwairith Radhi za Mwenyezi Mungu zimshukie kwamba Mtume (Saw) alisema:

وَصَلُّوا كَمَا رَأَيْتُمُونِي أُصَلِّي وَإِذَا حَضَرَتِ الصَّلَاةُ فَلْيُؤَذِّنْ لَكُمْ أَحَدُكُمْ ثُمَّ لِيَؤُمَّكُمْ أَكْبَرُكُم

Na swalini kama mlivyoniona nikiswali na inapowadia Swala, basi mmoja wenu aadhini kisha yule mkubwa wenu kiumri aweze kuwaswalisha.

Na akapokea Imam Ahmad kutoka kwa Abdullah Ibn Umar kuwa Mtume (Saw) alisema:

«أَقِيمُوا الصُّفُوفَ فَإِنَّمَا تَصُفُّونَ بِصُفُوفِ الْمَلَائِكَةِ وَحَاذُوا بَيْنَ الْمَنَاكِبِ وَسُدُّوا الْخَلَلَ وَلِينُوا فِي أَيْدِي إِخْوَانِكُمْ وَلَا تَذَرُوا فُرُجَاتٍ لِلشَّيْطَانِ وَمَنْ وَصَلَ صَفّاً وَصَلَهُ اللَّهُ تَبَارَكَ وَتَعَالَى وَمَنْ قَطَعَ صَفّاً قَطَعَهُ اللَّهُ»

Simamisheni safu kwani safu zenu zinakuwa pamoja na safu za Malaika na muoanishe bega kwa bega, zibeni mianya na wafanyieni upole ndugu zenu na wala msiache mianya ya shetani. Atakayeunga safu Mwenyezi Mungu Naye atamuunga na mwenye kukata safu Mwenyezi Mungu naye atamkata.

Ni bayana kutokana na dalili hizo hapo juu kwamba kuwalazimisha wenye kuswali kuweka umbali wa mita 1.5, sawa iwe ni swala za Ijumaa ama za Jamaa kwa hofu ya maambukizi hasa ikiwa wale waumini hawana dalili kabisa za maambukizi kitendo hiki ni uzushi katika Uislamu. Fauka ya haya, maradhi ya maambukizi ni udhuru wa kisheria wa Waislamu kutokwenda msikitini wala sio udhuru wa kuruhusu kwenda msikitini kisha kujiweka mita moja toka kwa mwengine wakati wa kuswali.

Kuhusiana na sharti la kuruhusu watu 100 pekee kuingia msikitini, kuwazuia watu wazima wenye umri wa 58 na watoto chini ya umri wa miaka kumi na tatu, kitendo hiki sio kuwa hakigongani tu na mafundisho ya Kiislamu bali pia dhulma dhidi ya waumini wa Kiislamu na ni jambo lisilomridhisha Mwenyezi Mungu SWT. Na mgongano mkubwa wa maadili ya uongozi kwa kuweka masharti magumu kwa wanaoswali ilhali barabarani, ofisini, madukani na maeneo mengine bado tunayaona yakifurika watu pasina masharti hayo ya umri. Je hii ina maanisha kwamba maradhi ya Covid-19 huweza tu kuambukizwa ndani ya Misikiti wala sio kwengineko na kwa hivyo ni lazima ifunguliwe kwa idadi maalumu ya waumini wenye umri maalum?!

Tunasisitiza kuwa janga hili ni changamoto na mtihani kutoka Muumba Aliyetukuka kwa waja wake ukitutaka kurudi Kwake Yeye kwa kwa kutubia na kunyenyekea kwa maamrisho yake. Kwa mnasaba huu, kufunguliwa kwa misikiti kwa masharti magumu ambayo yanagongana na sheria za Mwenyezi Mungu kunafanya vifua vya vya Waislamu kuungulika kwa maumivu makali. Hata hivyo, tunafahamu kwa yakini kuwa kwa kusimamisha tena Khilafah kupitia njia ya Utume katika moja ya mataifa makubwa ya Kiislamu, Misikiti hivi karibuni itatukuzwa na Jina la Mwenyezi Mungu kutajwa ndani yake asubuhi na jioni.

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo Vya Habari wa Hizb ut Tahrir Kenya

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kenya
Address & Website
Tel:  +254 707458907
E-Mail: mediarep@hizb.or.ke

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu