Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  29 Ramadan 1441 Na: 1441 H / 023
M.  Ijumaa, 22 Mei 2020

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Tangazo la Natija ya Kuuangalia Mwezi Mwandamo wa Shawwal 1441 H

Tahania kwa Sikukuu Iliyo Barikiwa ya Eid ul Fitr

Allahu Akbar, Allahu Akbar, Allahu Akbar, La Ilaha Ila Allah, Allahu Akbar, Allahu Akbar, Wa lilahi Alhamd
(Imetafsiriwa)

Bismillahi Ar-Rahman Ar-Raheem, Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola wa Walimwengu, mmiliki wa vipembe vyote vya ulimwengu; mwenye kutawala viumbe vyote. Rehma na amani zimshukie Mtume Wake, Muhammad Mtume wa Uislamu, Badr na Hijra na muasisi wa Dola na mwonyaji wa madhalimu, na Mtume wa vita vitukufu, bwana wa viumbe vyote, bwana wetu Muhammad, rehma na amani zimshukie yeye na jamaa na maswahaba zake…

Ahmad amepokea kutoka kwa Muhammad Bin Ziyad kwamba amesema, "Nimemsikia Abu Hurairah (ra) akisema: kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema, au alisema: Abu Al-Qasim (saw) amesema: «صُومُوا لِرُؤْيَتِهِ، وَأَفْطِرُوا لِرُؤْيَتِهِ، فَإِنْ غُبِيَ عَلَيْكُمْ فَعُدُّوا ثَلَاثِينَ» “Fungeni kwa kuonekana kwake (mwezi mwandamo) na fungueni kwa kuonekana kwake. Lakini ikiwa (kutokana na mawingu) utafichika kwenu basi hesabuni (siku) thalathini.”

Baada ya kuutafuta mwezi mwandamo wa Shawwal, usiku huu ulio barikiwa, mkesha wa kuamkia Jumamosi, imethubutu kuonekana kwa mwezi mwandamo kwa mujibu wa masharti ya Kisharia katika baadhi ya nchi za Kiislamu, na hivyo basi kesho, Jumamosi itakuwa ndio siku ya kwanza ya mwezi wa Shawwal na siku ya kwanza ya Idd ul-Fitr iliyo barikiwa.

Katika siku kuu hii iliyo barikiwa ya Idd ul-Fitr, Hizb ut Tahrir inatoa tahania zake za dhati kwa Ummah wote wa Kiislamu, salamu ambazo zinatoka ndani ya nyoyo za wabebaji ulinganizi wakweli, zilizo jaa matarajio yanayo tokana na bishara njema za Utume, na kuthibitishwa kupitia furaha inayo tukuza ibada ya Idd licha ya dhurufu zote.

Vilevile ninatoa tahania maalum kwa jina langu na jina la Mkuu wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir, na ndugu na dada wote wanaofanya kazi katika vitengo vyake kwa Amiri wa Hizb ut Tahrir, mwanachuoni mkubwa Sheikh Ata Khalil Abu Rashtah, nikimuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu amruzuku neema ya kuongoza Dawah hii ili kufikia bishara njema ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) kupitia kuasisi Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, na tamkini ya Ummah.

Idd imewasili na sisi bado tungali tunauona ulimwengu umezama ndani ya janga la maambukizi ya virusi vya Korona, na tungali tunaziona nchi za ulimwengu zikiongozwa na bwana wake muovu Amerika, zikitafuta mwanga wa matumaini ili kujinasua kutokana na "hofu ya kufungwa kiuchumi" ambayo imekuwa ndio hofu yao kubwa na jinamizi baya. Wanasayansi wao wanasema: "Endapo mutaufungua uchumi, maradhi haya yatawauwa!" Kisha matajiri wao wanajibu: "Endapo mutaufunga uchumi, njaa itawauwa!" Hivyo, baina ya hofu ya njaa na hofu ya maradhi, nchi za ulimwengu zinazurura zisipo pajua kwa janga hili. Mwenyezi Mungu (swt) asema,

 [وَضَرَبَ اللَّهُ مَثَلاً قَرْيَةً كَانَتْ آمِنَةً مُّطْمَئِنَّةً يَأْتِيهَا رِزْقُهَا رَغَداً مِّن كُلِّ مَكَانٍ فَكَفَرَتْ بِأَنْعُمِ اللَّهِ فَأَذَاقَهَا اللَّهُ لِبَاسَ الْجُوعِ وَالْخَوْفِ بِمَا كَانُواْ يَصْنَعُونَ]

“Na Mwenyezi Mungu amepiga mfano wa mji ulio kuwa na amani na utulivu, riziki yake ikiufikia kwa nafasi kutoka kila mahali. Lakini ukazikufuru neema za Mwenyezi Mungu; kwa hivyo Mwenyezi Mungu akauvika vazi la njaa na khofu kwa sababu ya yale waliyo kuwa wakiyafanya.” [Al-Nahl: 112].

Enyi watu:

Nchi za ulimwengu zimedhibiti janga la virusi vya Korona kwa mtazamo halisi wa kisekula wa kirasilimali, ambao daima wamedhani kuwa ndio unaotawala katika ulimwengu huu na viliyomo ndani yake, mwanzoni zililipuuza jambo hili, lakini zilipo shambuliwa, zilikabiliana na janga hili kupitia hatua ya kiidadi, ambapo ilizifanya kurudia alifu kwa ujiti kila wakati. Na ikiwa wamejifunza kuhusu "njia ya utume" ya hadhara ya Kiislamu na yanayo chipuza kutokamana nayo kuhusu maradhi, tauni na usafi, basi wangejua kwamba mtazamo ambao unastahili kuzingatiwa katika kukabiliwa na janga kama hili la maambukizi ni lazima uwe ule wa kibinadamu; imani yake, afya, pesa na maslahi, na hili lawajibisha kutafuta umalizaji kikamilifu wa janga hili, na sio tu kupunguza idadi ya walio athirika pekee. Njia ya utume inahitaji kwamba, pindi tu maradhi yanapo sikika, utengaji wa maeneo ya kijografia huanza ndani ya nchi, hivyo ni haramu kutembea baina ya maeneo ambako kuna maambukizi na ambako hakuna.

Kisha wagonjwa walio athirika wanatengwa kutoka kwa watu walio wazima, na maisha yanaendelea katika maeneo ambayo hakuna maambukizi, na wagonjwa wote wanapewa uangalizi bila malipo na kwa gharama ya dola. Juhudi zinaendelea kuzuia janga hili hadi lifikie "hakuna visa vya maambukizi", na sio kufunga nchi nzima au kufungua nchi nzima, au kufunga nchi nusu au kufungua nchi nusu, au kulazimisha marufuku kamili ya kutotoka nje, au marufuku nusu ya kutotoka nje. Hatua zote hizi huchelewesha kile kinacho julikana, yaani kila watu wanapo changanyika, maambukizi yatarudia kusambaa.

Ingawa idadi ya vyombo vya habari vya Kimagharibi na vile vilivyoko katika nchi yetu vimevutia umakinifu wa nchi kwa mtazamo wa Uislamu wa utume, ambao tumeutaja, na licha ya ukweli kuwa Uislamu ni hadhara ambayo ni ya zamani zaidi kuliko hadhara ya Magharibi, Magharibi imeuchukua Uislamu kama adui na kujitia uziwi wa uzuri wake na kuamua kukabiliana na hatma yake huku ikimsahau Mola wake! Mwenyezi Mungu (swt) asema:

 [فَلَمَّا نَسُواْ مَا ذُكِّرُواْ بِهِ فَتَحْنَا عَلَيْهِمْ أَبْوَابَ كُلِّ شَيْءٍ حَتَّى إِذَا فَرِحُواْ بِمَا أُوتُواْ أَخَذْنَاهُم بَغْتَةً فَإِذَا هُم مُّبْلِسُونَ]

“Basi walipo sahau walio kumbushwa tuliwafungulia milango ya kila kitu. Mpaka walipo furahia yale waliyo pewa tuliwashika kwa ghafla, na mara wakawa wenye kukata tamaa.” [Al-An’am: 44].

Enyi Waislamu:

Mwezi wa Taraweh umepita huku mukiharamishwa kuswali misikitini mwenu! Nyumba za Mwenyezi Mungu hazikufunguliwa kwenu, kwa sababu watawala wenu wanafuata Magharibi, ambao hawathamini imani yenu au Shariah yenu. Hawaoni haja ya sehemu za ibada huku wakitukuza haja ya mabenki na masoko! Vilevile, watawala vikaragosi, waliolishwa kasumba ya kutazama chochote kinacho husiana na Uislamu kuwa duni, na kuifunga misikiti kwa taratibu na kamwe hawakutafari kuhusu namna ya kuiwacha wazi huku wakichukua hatua za tahadhari, kama walivyo fanya kwa sehemu nyenginezo walizozifungua! Wanazuoni wa kiserikali walikuwa haraka zaidi kuwashinda wao kuwahami kwa fatwa munasib ili kuwagandamizeni. Hata baadhi ya wanazuoni walisubutu kuharamisha ufunguzi wa nyumba za Mwenyezi Mungu! Mwenyezi Mungu (swt) asema:

 [وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّن مَّنَعَ مَسَاجِدَ اللَّهِ أَن يُذْكَرَ فِيهَا اسْمُهُ]

“Na ni nani dhaalimu mkubwa kuliko yule anaye zuia misikiti ya Mwenyezi Mungu kutajwa ndani yake jina lake” [Al-Baqara: 114]

Enyi Ummah bora ulioletwa kwa wanadamu:

Kamwe haijawahi kutokea katika historia ya Ummah huu wanazuoni kusubutu kuharamisha kwenda katika nyumba za Mwenyezi Mungu! Haitoshi kusema kuwa je, hii ndio Ramadhan ya kwanza katika historia ya Ummah huu tangu ujumbe wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), ambao Ummah wa Kiislamu umezuiwa kutokana na kuswali misikitini?! Haitoshi kwa sababu ya yale yaliyo tokea ili kuigeuza meza ya mfumo huu uliooza na kuubadilisha kwa nidhamu ya Uislamu, ilhali nyinyi ni Ummah wa idadi ya (watu) bilioni mbili?!

Hakika, naapa kwa Mwenyezi Mungu inatosha kufanya hivyo na zaidi, inatosha kwenu kurudisha Dola ya Khilafah haraka iwezekanavyo, na kwenda kwa watu wa Magharibi ambao wamesambaratishwa na nchi zao na kuwapa amana ya Mola wenu, ambayo ni Dini ya Uislamu na uwezo wake wa kuwaokoa wanadamu, Mwenyezi Mungu Mtukufu asema:

 [وَكَذَلِكَ جَعَلْنَاكُمْ أُمَّةً وَسَطاً لِّتَكُونُواْ شُهَدَاء عَلَى النَّاسِ]

“Na vivyo hivyo tumekufanyeni muwe Umma wa wasitani, ili muwe mashahidi juu ya watu,” [Al-Baqara: 143].

Kwa Waislamu wote popote walipo:

Hizb ut Tahrir inawasihi kwa maneno ya Mwenyezi Mungu (swt), kwa Seerah ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), kwa fikra angavu, na kwa hali ambazo ulimwengu umefikia; Njooni mufanye kazi kusimamisha Khilafah, njooni mufanye kazi kwa ajili ya mama wa faradhi zote katika Uislamu, njooni ili muweze kuregea kuwa Ummah bora ulioletwa kwa wanadamu…

Allahu Akbar, Allahu Akbar, Allahu Akbar, La Ilaha Ila Allah, Allahu Akbar, Allahu Akbar, Wa lilah Alhamd.

Idd Mubarak, Wassalamu Alaikum Wa Rahmatullah Wa Barakatuh.

Mkesha wa kuamkia Jumamosi ndio siku ya kwanza ya mwezi wa Shawwal ya mwaka wa 1441 Hijria sawia na 23/5/2020.

Mh. Salah Eddine Adada
Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.