Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  29 Rajab 1442 Na: 026 / 1442 H
M.  Ijumaa, 12 Machi 2021

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Hitimisho la Kampeni "Katika Kumbukumbu ya Karne Moja ya Kuvunjwa kwa Khilafah… Isimamisheni Enyi Waislamu"

(Imetafsiriwa)

Kwa msaada wa Mwenyezi Mungu (swt), leo tunahitimisha kampeni ya kiulimwengu iliyozinduliwa na Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut-Tahrir chini ya uongozi wa Amiri wa Hizb ut-Tahrir, mwanachuoni mkubwa, Ata bin Khalil Abu Al-Rashtah, kwa mnasaba wa kumbukumbu ya miaka 100 ya kuondolewa kwa Khilafah, ambapo kampeni hii ilifanywa kwa ushirikiano na kwa njia ya Utume kote ulimwenguni.

Pamoja na tangazo la kuanza kwa kampeni, shughuli na amali za habari zilianza, ambazo zililenga nchi kadhaa ulimwenguni. Na kwa kuwa nchi nyingi ambazo shughuli za kampeni zilifanyika bado zinateseka chini ya mzigo wa janga la Korona, amali hizi zilifanywa kwa mujibu wa hatua za tahadhari za usalama wa umma. Visimamo, kalima za video, semina na mihadhara, mahojiano ya moja kwa moja, makala na taarifa, zilichapishwa na kutangazwa kwenye tovuti na vituo vya habari.

Kalima na visimamo vilifanywa mbele ya majengo ya kihistoria ya Khilafah katika nchi za Kiislamu ili kuelezea ukubwa wa kumbukumbu hii, kiwango cha shauku ya Umma na hamu ya kurudi kwake, kwa hivyo uliungana tena na kukusanya maeneo yake na kuondoa sababu za mgawanyiko wake ambao wakoloni walikuwa wameugubika baina ya wanawe, na kurudisha utukufu wao, na kutabikisha sheria yao, na kusimamia mambo yao haki ya usimamizi, na kuyarudi madai ya maadui, na kunyanyua bendera ya Tauhid juu ya ardhi yao kama vile alivyoinyanyua na Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) na maswahaba zake watukufu (ra), siku waliposimamisha dola ya kwanza ya Waislamu, na wakawashinda Waajemi na Warumi, watawala wa ulimwengu wakati huo, chini ya kivuli chake na wakaeneza Uislamu na dawah na kwa kweli wakawa Umma uliotolewa kwa watu.

Kilele cha kampeni hii kilikuwa ni kalima ya Amiri wa Hizb ut Tahrir, Mwenyezi Mungu amhifadhi, iliyokuwa na maana kubwa sana ambayo alielekezwa kwa Umma wa Kiislamu, kwa hivyo aliukumbusha kupitia kalima hii faradhi kubwa, faradhi ya kusimamisha Khilafah na akabainisha dalili za Sharia katika hilo na yaliyomo katika jambo hili la umuhimu mkubwa kwa Umma wa Kiislamu na wengine vilevile.

Wito na mialiko iliyokuja katika kalima, makongamano, matoleo, na visimamo vyote kwa jumla vilikuwa na wito wa moja kwa moja kwa Umma wa Kiislamu na majeshi yake kurudi kwenye utukufu na izza hiyo ambazo zilikuweko chini ya kivuli cha dola ya Khilafah na hukmu ya Sharia ya kweli, na kwamba Hizb ut-Tahrir imeonyesha njia ya kurudi kwenye fadhila hii kubwa na bado ingali inafanya kazi na Ummah ili kuuondoa kutokana na kufuata nidhamu za kikafiri zilizowekwa na wakoloni makafiri wa Magharibi.

Vilevile, sisi katika afisi kuu ya habari ya Hizb ut Tahrir, tunatuma ombi la dhati kwa kila Muislamu mwenye ghera na Uislamu ambaye anafanya kazi katika vyombo vya habari, kushiriki katika usambazaji wa juhudi hii iliyofanywa kwa kumridhisha Mwenyezi Mungu (swt), na kuchangia katika dori yake dawah ya kurudi kwa utukufu wa Waislamu, dawah ya kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa Njia ya Utume.

#أقيموا_الخلافة

#ReturnTheKhilafah

#YenidenHilafet

#خلافت_کو_قائم_کرو

Mh. Salah Addine Adada

Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir 

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.