Alhamisi, 18 Ramadan 1445 | 2024/03/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Jibu la Swali
Kujiondoa kwa Amerika Kutoka Katika Mkataba wa Makombora Pamoja na Urusi

(Imetafsiriwa)

Swali:

Waziri wa Kigeni wa Amerika alitangaza rasmi mwanzoni mwa mwezi huu kujiondoa kwa Amerika kutoka katika Mkataba wa INF (Nguvu za Kinuklia za Masafa ya Kati na Kati – upunguzaji wa makombora ya masafa ya kati na kati na masafa mafupi) uliotiwa saini pamoja na Urusi mnamo 1987. Ni vipi vipimo vya kujiondoa huku kwa Amerika? Je, Urusi kweli ilikiuka mkataba huo au ni kisingizio tu cha Amerika kujiondoa? Ikiwa Urusi haikukiuka mkataba huo, basi ni yapi malengo ya kujiondoa huku na ni kwa nini imejiondoa? Allah akujazi kheri.

Jibu:

ili kupata jibu la wazi, tunaregelea yafuatayo:

Kwanza: Ndio, “Waziri wa Kigeni wa Amerika Mike Pompeo alisema mnamo Ijumaa kuwa Amerika huenda ikasitisha uwajibikaji wake kwa marufuku ya makombora ya masafa mafupi na masafa ya kati na kati pamoja na Urusi. Alisema: “… Amerika iliipatia Urusi na washirika wengine wa mkataba huo ilani rasmi kuwa Amerika itajiondoa kutoka katika Mkataba wa INF ndani ya miezi sita.” Alithibitisha kuwa nchi yake itasitisha dori yake chini ya Nguvu ya Kinuklia ya Masafa ya Kati na Kati kuanzia Jumamosi. “Alitishia kuwa “Kwa mujibu wa Kanuni ya Kijamii ya Kimataifa, Amerika imesitisha wajibu wake chini ya Mkataba wa INF,” (state.gov; Arabic 21, 1/2/2019). Tangazo hili la Amerika lilitarajiwa baada ya Amerika kuibua shaka miezi kadhaa iliyopita kuhusu uwajibikaji wa Urusi katika Mkataba wa INF. Trump alisema: “Amerika haitaiacha Urusi “kutengeza silaha ambazo haturuhusiwi kutengeza.” (BBC, 21/10/2018)

Urusi ilishtushwa kwa hatua hii. Naibu Waziri wa Kigeni wa Urusi Sergei Ryabkov alisema: “Hii itakuwa ni hatua hatari mno na itachochea shutuma kali.” Aliliambia Shirika la Habari la TASS kuwa mkataba huo ni muhimu kwa ajili ya usalama wa kiulimwengu katika mazingira ya mbio za kisilaha na ili kuhifadhi amani ya kimikakati. Ryabkov alikashifu kile alicho kiita “Majaribio ya Amerika kupata maridhiano kupitia vitisho” (BBC, 21/10/2018). Baada ya kujulishwa rasmi kujiondoa kwa Amerika, Urusi ilijibu kwa hatua sawa na hiyo. “Katika taarifa kwa vyombo vya habari mjini Ashgabat,” Lavrov alisema: “Raisi Vladimir Putin ameweka msimamo wetu kuwa tujibu kwa njia hiyo hiyo,” akiongeza kusema: “Waamerika wamesitisha kujitolea kwao kwa mkataba huo, na sisi tumefanya hivyo hivyo, na mwishoni mwa muda wa miezi sita uliopeanwa katika mkataba huo, na kutokana na ujumbe rasmi wa Amerika juu ya kujiondoa kwa Washington katika mkataba huo, sisi pia tutaumaliza.” (RT, 6/2/2019). Hivyo basi ni wazi kuwa Amerika kwa hakika inajiondoa kutoka katika makubaliano hayo, hata kabla ya kumalizika kwa muda wa miezi sita, na imetangaza kuwa itaanza miradi ya utafiti na makombora iliyo zuiwa na Mkataba huo …

Pili, sababu ya kujiondoa kwa Amerika ni ile ambayo imeitangaza; kuwa kupitia utengezaji wa Urusi wa kombora aina ya 9m729, makubaliano hayo yamekiukwa. Hii si kweli na kuna shaka. Urusi ilitangaza kuwa kombora lake lina masafa ya kilomita 480, yaani chini ya masafa ya kilomita 500 ambayo yamepigwa marufuku katika makubaliano hayo. Makubaliano hayo yametaja marufuku hiyo ya makombora ya masafa mafupi ya kilomita 500 hadi kilomita 1000, na masafa ya kati na kati ya kilomita 1000 hadi kilomita 5500. Makombora ya Urusi, ya kiwango cha masafa mafupi na masafa ya kati na kati, hayatishii eneo la Amerika moja kwa moja. Bali Muungano wa Kisovieti, ambao ulikuwa umezungukwa na maadui wengi, ulizalisha idadi kubwa ya makombora haya ambayo haswa yanaweza kufika Ulaya Magharibi. Pindi Amerika ilipo anzisha makombora ya Pershing na Cruz mnamo miaka ya themanini, katika Ulaya Magharibi, Muungano wa Kisovieti ulijibu kwa kuunda makombora aina ya S-20 ya masafa ya kati na kati. Ulaya ikawa ndio uwanja unaotarajiwa zaidi wa vita vya kinuklia kati ya Amerika na Muungano wa Kisovieti katika miaka ya themanini, kwa hivyo imeingiwa na hofu na kushinikiza kutamatishwa kwa makubaliano hayo ili kupunguza makombora ya masafa ya kati na kati.  

Tatu, kwa kuiangalia hatua ya Amerika wakati huo, hatari ya sera ya Amerika inawezekana kufahamika. Kwa upande mmoja, Amerika imeongeza fungamano lake la kiusalama pamoja na Ulaya Magharibi na kuifanya hatima ya bara la Ulaya kutegemea Washington. Kwa upande mwengine, Amerika imeona kuporomoka kwa hatua zake za kuondoa silaha tangu mwanzoni mwa miaka ya themanini, na baada ya majadiliano ya kuondoa silaha na kupitisha makubaliano kati ya nchi mbili hizo, Amerika imelenga hususan juu ya makombora ya masafa mafupi na masafa ya kati na kati. Ili hasara kubwa iwe kwa Muungano wa Usovieti, ambao uliangamiza makombora ya kinuklia 1,800, ambayo uliyafadhili, huku Amerika ikiangamiza roketi 800 pekee, yaani chini ya nusu yale yaliyo angamizwa na Moscow. “Kufikia May 1991 pande mbili hizo zilitangaza kuharibu zaidi ya makombora 2600 katika kutekeleza Mkataba huo, hisa ya Urusi ilikuwa takriban roketi 1800.” (Al Jazeera.net 2/2/2019). Kwa maana nyengine, Mkataba huo wa kuangamiza makombora ulimalizika mnamo 1991, na kujitolea kwa makubaliano hayo, yaani, kujizuia kutokana na kutengeza makombora ya kinuklia sawa na hiyo, kungalipo.  

Nne, kwa mkakati huo wa Amerika wa utawala wa Trump na nusu yake kukubaliwa na utawala wa Obama uliopita, yaweza kuonekana kuwa yanayojiri ulimwenguni yameilazimisha Washington kuzingatia upya sera jumla ya Amerika … Kadhia za kina ambazo mkakati wa Amerika unalenga kutatua ni: 

1 - Uchumi wa Amerika: Amerika inaona uchumi wake kama mojawapo ya nguzo za nguvu yake ya kimataifa umedhoofika kimataifa … Lakini, imegundua kuwa Ulaya iko imara kiuchumi kwa sababu haigharamikii vya kutosha juu ya usalama, kwa kuwa imedhaminiwa kupitia mwavuli wa kiusalama wa Amerika … Kwa upande mwengine, sio muhimu kuliko Ulaya, kuinuka kwa China kulikuwa kwa haraka mno. China iliunda uchumi wa hali ya juu kwa muda wa miongo miwili tu, na kuunda taasisi za kifedha kama vile Benki ya Maendeleo ya Asia, huku ikitishia hadhi ya taasisi za kimataifa zilizoundwa na Amerika, kama vile Benki ya Dunia …

Ukweli huu na ukosefu wa ustawi kwa uchumi wa kimataifa yameifanya Amerika kuwa na wasiwasi na mustakbali wa uchumi wake kama msingi wa utawala wake wa kiulimwengu. Kwa hivyo imeangazia juu ya nguvu yake ya kijeshi na kutoa makucha yake ya kinuklia na ya makombora ili kuhofisha nchi washindani. Amerika chini ya Trump haikuficha malengo yake. Raisi wa Amerika alisema, “… nchi yake huenda ikaongeza zana zake za kinuklia ili “wengine watie akili” (CNN; Al-Youm As-Sabi’ 6/11/2018)

2- Miondoko ya Ulaya dhidi ya Amerika: Raisi wa Ufaransa Macron alitoa wito wa kuasisiwa jeshi la Ulaya ili kusimama dhidi ya miondoko ya Urusi na China, hata ya Amerika. Trump alishangazwa na jinsi Ulaya inavyo weza kufikiri kuwa Amerika inasimama kama tishio kwa usalama wake wakati ndiyo inayoifinika kivuli na kulinda usalama wake na kugharamia ulinzi wake. Ulaya inaipinga Amerika katika nyanja nyingi kama vile makubaliano ya anga, vita vya Amerika juu ya Iraq, na mivutano ya kiushawishi katika maeneo ya Kiarabu, Kiislamu na Afrika, na Ulaya inashirikiana pakubwa pamoja na China …Kwa yote haya, Amerika inalitaka tishio la Urusi ili kuifanya Ulaya itie akili. Kupitia kujiondoa kutoka katika makubaliano pamoja na Urusi, Urusi italazimika kutengeza makombora na tishio la nuklia la Urusi litahamishwa Ulaya, inayopakana na Urusi ambako mkataba huo uliundwa wa kukomesha ushindani wa kinuklia juu ya ardhi ya Ulaya. Waziri wa Kigeni wa Ujerumani Heiko Maas alisema katika taarifa iliyo nukuliwa na waandishi wa habari wa Reuters, “Kwa miaka 30 Mkataba huo ulikuwa ndio msingi wa usalama wa Ulaya” (Sputnik, Russian, 21/10/2018).

Heiko Maas aliliambia shirika la habari la Deutsche Presse-Agentur dpa, “Nchi yake itapinga vikali hatua yoyote ya kutumia makombora ya kinuklia ya masafa ya kati na kati barani Ulaya,” katika mahojiano yaliyo chapishwa mnamo Jumatano, shirika hilo lilimnukuu akisema, “Katika hali yoyote Ulaya haipaswi kuwa jukwaa la mdahalo wa kujihami kisilaha.” (Reuters; Al-Wifaq Online 28/12/2018) Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alisema mwanzoni kuwa “kujiondoa kwa Amerika kutoka katika Mkataba huo wa kupunguza makombora ya masafa ya kati na kati na masafa mafupi kutahatarisha usalama wa Ulaya. Macron aliiambia redio ya Ufaransa, ya Europe 1 French, mnamo Jumanne, “Pindi ninapomuona Rais Trump akitangaza kuwa anajiondoa kutoka katika mkataba wa kuondoa silaha … mwathiriwa mkuu ni nani?” (Al-Youm As-Sabi’ 6/11/2018).    

3- Sera ya Urusi na shinikizo la Amerika juu yake: Baada ya idara ya Trump kuingia mamlakani nchini Amerika, hakuna hata mwezi mmoja unapita bila ya kuongeza shinikizo la Amerika juu ya Urusi, kuanzia kwa vikwazo na kufungwa kwa muundo wa kijeshi wa NATO kutoka mipakani mwa Urusi, kuunganishwa kwa nchi mpya za NATO (Macedonia), kujihusisha kwa Urusi nchini Syria, na kuunganishwa kwa nidhamu dhidi ya makombora katika mpaka wake wa mashariki (nchini Korea Kusini), hata shinikizo la mwisho la Amerika halileti uhai kwa Japan kudai Visiwa vya Kuril na mgogoro wa mahusiano ya Urusi na Japan … kilichoifanya Amerika kuwa na ukakamavu zaidi dhidi ya Urusi ni mwitikio wa Urusi kwake nchini Syria.

Amerika inataka kugurisha huduma ya kimataifa ya Urusi kwa Amerika hadi maeneo ya China. Urusi inafahamu hili vizuri mno. Waziri wa Kigeni wa Urusi Sergei Lavrov alikuwa mukhlis pindi alipo thibitisha kuwa Amerika haitaweza kuigeuza Urusi kuwa ala ili kutumikia maslahi yake na kupambana na China. Alisema, “Wanafanya kazi kutufanya tuwe adui ili kulazimisha indhibati juu ya Ulaya na kuimarisha mafungamano kati ya Ulaya na Atlantiki, kwa mfano, sasa wanajadiliana kwa umakinifu jinsi Urusi itakavyoitumia China ili kuwanufaisha wao … katika hamu yao ya kutufanya kuwa ala ili kutumikia maslahi ya Amerika.” (RT, 24/12/2018) 

Urusi, baada ya Amerika kufanikiwa kuihusisha nchini Syria ili kutumikia maslahi ya Amerika sasa iko chini ya shinikizo kubwa la kuburuzwa dhidi ya China, na huu ni msitari mpana katika sera mpya ya Amerika katika muondoko wa Urusi … Kupitia kujiondoa kwa Amerika kutoka katika Mkataba huo wa makombora ya masafa ya kati na kati na masafa mafupi pamoja na Urusi, inaongeza shinikizo juu ya Urusi kwa upande mmoja, na upande mwengine ina vuruga mahusiano yake na China: kuongeza shinikizo juu ya Urusi ni kupitia kuisukuma katika mbio mpya za kisilaha ambazo uchumi wake hauziwezi, alisema Naibu Waziri wa Kigeni wa Urusi Sergei Ryabkov. “Hatutaki kujihusisha katika mbio za kisilaha pamoja na Amerika huku ikijaribu kutuburuza humo.” (RT Arabic, 7/2/2019) Ama kuhusu kuvurugika kwa uhusiano na China, Amerika kupitia kuilazimisha Urusi, kutangaza mbio za kisilaha katika zana za kimikakati za kati na kati na fupi itasababisha shauku kuu nchini China inayopakana na Urusi. Eneo lote la China litakuwamo ndani ya masafa ya makombora hayo, yaliyoimaliza Urusi kufikia 1991, na hili linaibua taharuki kati ya China na Urusi.

4- Kukua kukubwa kwa China na kile ambacho Amerika inahitaji ili kupambana nayo: Sera mpya ya Amerika, ambayo imekuweko tangu muhula wa pili wa Obama, inaiweka China juu zaidi ya vipaombele vya Amerika. Trump amedumisha kipaombele hiki. Anapigana vita vya kibiashara pamoja na China ili kukomesha kukua kwake, hususan kwa kuwa nguvu ya kiuchumi ya China inaifanya kuwa na uwezo wa kuunda jeshi imara lisilo kosa silaha za kinuklia, na huenda ikaendelea na kusababisha hatari zaidi kwa nguvu ya Amerika na utawala wake. Bajeti ya jeshi iliyo tangazwa na China ($ 228 bilioni) ni kubwa kuliko bajeti za jeshi za nchi hizi nne zinazofuata China (Urusi, Uingereza, Ufaransa na Ujerumani kwa jumla) na Amerika haipuuzi uwezekano kuwa China inaficha baadhi ya mipango yake ya kijeshi, huku uchumi wake ukijitayarisha kwa matumizi zaidi ya kijeshi. Kwa upande mmoja, Amerika, iliyo vurugwa kutokana na vita vya kiuchumi pamoja na China, kwa sababu ya kuja pamoja kwa nguvu ya mbili za kiuchumi, inataka kusongeza juhudi zake ili kudhibiti kukua kwa China katika uwanja wa kijeshi ambao bila shaka Amerika ina nguvu zaidi ikilinganishwa na China.    

Hii ni kwa sababu Amerika inataka kuvunja vikwazo (mkataba wa makombora pamoja na Urusi), ambavyo vinaizuia kutokana na kuizunguka China kwa silaha za kinuklia za masafa ya kati na kati na masafa mafupi ambazo inaweza kuziweka Korea Kusini, Japan na nchi nyenginezo pambizoni mwa China … Kwa maana nyengine, inataka kuvuruga nguvu ya kiuchumi ya China kupitia kuisukuma katika mbio za kisilaha. China inatengeza makombora zaidi ya masafa ya kati na kati na masafa mafupi katika kujibu uwezekano wa hatua za Amerika katika maeneo yanayoizunguka China, katika muda ambao Amerika haitumii tu uwezo wake wa kiuchumi lakini pia ule wa Japan na Korea Kusini katika mbio za kisilaha za Mashariki ya Mbali. Hili limeisukuma China kuanguka kutoka katika kiwango chake cha sasa.  

Tano: Kwa kutamatisha, malengo ya muda mrefu ya Amerika yamekuwa wazi kupitia kujiondoa kutoka katika makubaliano ya makombora pamoja na Urusi kama ifuatavyo:

1- Kwa kuanguka uchumi wa Amerika na udhaifu wa nguvu yake kama chombo kikuu cha utawala wa Amerika, hususan kwa kukua uchumi wa China na uhasimu wake kwa uchumi wa Amerika, pamoja na ushindani wa Ulaya, Amerika imeamua kuongeza uwezo wake wa kimikakati wa kijeshi ambao hakuna yeyote atakaye pambana nao, ili kutatua na kumakinisha utawala wake wa kimataifa barani Ulaya na pamoja na Urusi na China.

2- Kwa kuendelea kukua kwa mgawanyiko wa Ulaya na mizozo ya kisiasa ya Ulaya pamoja na Amerika katika nyingi ya kadhia za kimataifa, Amerika imeamua kuliregesha tena tishio la Urusi ili kuupa mzigo upya upande wa Ulaya, kama ilivyokuwa zama za Usovieti, kupitia kuunda upya mbio za kisilaha pamoja na Urusi ili kuzilazimisha nchi za Ulaya kuchagua kuwa chini ya mwavuli wa Amerika ili kuilinda kutokana na Urusi, na hivyo basi kukubaliana na masharti mapya ya Washington kama vile kuongeza matumizi katika jeshi na kuhakikisha kudumu kwake chini ya uongozi wa Amerika.

3- Kuongeza shinikizo juu ya Urusi, na kutishia msimamo wa kimikakati ulioko sasa kupitia kwa mbio mpya za kisilaha ambazo Urusi haiwezi kuzimudu, na kuilazimisha kuchukua misimamo ambayo hairidhishi China, ambayo inasababisha mgawanyiko baina ya nchi mbili hizo. Chini ya msimamo mpya wa kimikakati uliolazimishwa kupitia kujiondoa kwa Washington kutoka katika mkataba huo, Urusi ina machaguo mawili: moja ni chungu zaidi kuliko jengine, ima kuendelea na mbio za kisilaha zilizo feli zinazo dhihirisha uchache wa uwezo wake wa kimikakati, ikisongea karibu zaidi na msimamo wa Ufaransa na Uingereza kwa upande wa uwezo wa kimikakati, au kujibu shinikizo la Amerika ili iweze ‘kuokoa uso’ na hivyo basi kudumisha ukubwa wa kimataifa unaotegemea kikamilifu kukubali kwa Amerika, kwa badali ya kuifuata Amerika ili kutumikia malengo yake pambizoni mwa China.

 4- Katika upande wa China, malengo ya Amerika ya kujiondoa kutoka katika mkataba wake pamoja na Urusi huenda ikawa katika kipaombele cha kwanza cha Urusi. Amerika inataka kudhibiti uwezo wa kijeshi wa China, na haitaki kupigwa na mshangao kupitia uwezo huo, kama ilivyo pigwa na mshangao na kukua kwa haraka kwa uchumi wa China … Hii itakuwa kwa kupitia kudhibiti uwezo huo, kupitia kuweka mikataba ili kukua kwake kuwe chini ya macho na uangalizi wa Amerika, au kuilazimisha China kuanza mbio za kisilaha za kimikakati katika eneo la Mashariki ya Mbali. Mbio ambazo Amerika ina nguvu juu yake, na kuzifanya kuwa ni chombo chenye nguvu katika kuvunja nguvu ya uchumi wa China, na hivyo kuisukuma katika kushuka chini kwake.

Sita: Katika kutamatisha, kinacho vunja moyo ni kuwa Waislamu wako mbali na uwanja wa mzozo huu wa kimataifa, hawamo! Bali watawala waangamivu katika biladi za Kiislamu wanaiitikia zaidi Amerika hususan na Magharibi kwa jumla ili kulizuia zimwi la Uislamu kutokana na kuzuka kwake …

Lakini kuongezeka kwa nishati ya Ummah wa Kiislamu kwa Uislamu na kuzikataa mbinu za watawala masekula na harakati dhidi yao, ni thibitisho kuwa zama za utawala wa kiimla haziko mbali kumalizika, na zitabadilishwa kupitia Dola ya Khilafah Rashidah kupitia mikono ya wafanyakazi wenye ikhlasi na kunali bishara njema ya Mtume (saw): 

«ثُمَّ تَكُونُ مُلْكاً جَبْرِيَّةً فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ تَكُونَ ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ ثُمَّ سَكَتَ»

“kisha utakuwepo utawala wa kiimla utakuwepo katika muda apendao Mwenyezi Mungu uwepo kisha atauondoa atakapo taka kuuondoa, kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume.”

Na kisha nuru ya Khilafah itang’aa tena duniani na wakoloni makafiri watakimbia na maovu yao hadi makwao, na Ummah wa Kiislamu utarudi tena kuwa kama kiongozi wa ulimwengu ukiwa mbali na uovu na watu wake.

 (وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللَّهِ يَنْصُرُ مَنْ يَشَاءُ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ)

“Na siku hiyo waumini watafurahi* Kwa nusra ya Mwenyezi Mungu humnusuru amtakaye na Yeye ni Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu” [Ar-Rum: 4-5]

07 Jumada II 1440 H
Jumanne, 12/02/2019 M

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoAlhamisi, 02 Aprili 2020 20:59

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu