Ijumaa, 19 Ramadan 1445 | 2024/03/29
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Vichwa vya Habari 30/9/2020

Vichwa vya Habari:

NATO ya Asia

Nagorno-Karabakh Walipuka

Waziri Mkuu Mteule wa Lebanon Ajiuzulu

Maelezo:

NATO ya Asia

Naibu Waziri wa Kigeni wa Amerika Stephen Biegun amedokeza kuwa ushirikiano usio rasmi kati ya Amerika, Australia, Japan, na India unaweza kuwa mwanzo wa mtindo wa muungano wa NATO katika eneo la Indo-Pasifiki. Nchi hizo nne, zinazojulikana kama Quad, tayari hufanya mazoezi ya kijeshi ya pamoja ya mara kwa mara katika Pasifiki. Mnamo Agosti 31, Biegun alizungumza kwenye mazungumzo ya kimkakati ya Amerika na India na kujadili uwezekano wa kuunda muungano kama huo pamoja na Quad. "Ni ukweli kwamba eneo la Indo-Pasifiki kihakika linakosa miundo thabiti ya pande nyingi. Hawana chochote cha nguvu za NATO au Muungano wa Ulaya," Biegun alisema. "Kwa yakini kuna mwaliko huko katika wakati fulani ili kurasimisha muundo kama huu." Itifaki nchini Amerika ni China ndio tishio la kwanza kwa ubwana wa kiulimwengu wa Amerika. Hii imesababisha Amerika kufikiria kuunda muungano wa aina ya NATO barani Asia ili kukabiliana na China inayokua.

Nagorno-Karabakh Walipuka

Mapiganao yalizuka baina ya Azerbaijan na Waarmenia wanati katika eneo linaloshindaniwa la mlima wa Nagorno-Karabakh. Maafisa huko Nagorno-Karabakh walisema wanajeshi wao 26 zaidi waliuawa na kufanya jumla ya wanajeshi waliokufa wa Nagorno-Karabakh kufikia 84. Raia kumi na moja wameripotiwa kuuawa katika mapigano hayo, tisa upande wa Azerbaijan, na wawili upande wa Armenia. Armenia na Azerbaijan, zote ni dola mbili za baada ya Usoviet, zimefungwa katika mzozo wa kieneo juu ya Nagorno-Karabakh kwa miongo kadhaa. Mapigano haya yanahatarisha kuchochea mzozo mpana wa kikanda, huku Uturuki ikitoa msaada wake nyuma ya Azerbaijan. Siku ya Jumatatu, Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alitaka Armenia imalize "kuikalia" kwake Nagorno-Karabakh. Urusi ina makubaliano ya pamoja ya ulinzi na Armenia na ina kambi za kijeshi nchini humo. Lakini Moscow pia inafurahia uhusiano wa kirafiki na Azerbaijan na haionekani kuwa na hamu kuingia katika mzozo huo. Urusi imezisihi pande zote mbili kujizuia na ikatoa wito wa kusitishwa kwa mapigano huko Nagorno-Karabakh.

Waziri Mkuu Mteule wa Lebanon Ajiuzulu

Katika hotuba iliyopeperushwa katika runinga, Waziri Mkuu mteule wa Lebanon Mustafa Adib alitangaza kujiuzulu chini ya mwezi mmoja baada ya kuteuliwa kwenye nafasi hiyo mnamo Agosti 31 kuunda serikali. Lebanon inakabiliana na migogoro mingi ya kisiasa na kiuchumi. Mlipuko wa Bandari ya Beirut ulizua hasira miongoni mwa raia wa nchi hiyo, ambao wamekuwa wakidai mabadiliko. Uundaji wa serikali ya Lebanon kwa mara nyengine tena umesambaratika kwa sababu ya mapigano ya kimadhehebu, ambayo yamefanya kukaribia kutowezekana kupitisha maamuzi yoyote makubwa ya serikali, achilia mbali mabadiliko mapana ya kisiasa yanayohitajika. Kizuizi kimoja kikubwa wakati huu kilikuwa ni mzozo kati ya viongozi wa nchi hiyo wa Kishia na wenzao wa Kisunni na wa Kikristo juu ya jaribio la waziri mkuu huyu wa zamani la kuendelea kushikilia umiliki wa wizara ya fedha yenye faida.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu