Logo
Chapisha ukurasa huu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Vichwa Vya Habari 24/07/2020

 Vichwa vya habari:

Uhasama Mpya kati ya Amerika na China Utaulazimisha Ulimwengu kuchagua upande

Pakistan Yatoa Onyo la Mwisho kwa TikTok juu ya Maudhui Machafu

Ufaransa Yaungana na Amerika, Uingereza katika Kuishutumu China kwa Mateso ya Waislamu wa Uighur

Maelezo:

Uhasama Mpya kati ya Amerika na China Utaulazimisha Ulimwengu kuchagua upande

Pindi dola mpya inapoibuka ili kuipiku dola iliyopo, vurugu na mchuano haviepukiki — Hivyo ni muda tu kabla ya Amerika na China kupigana. Tofauti kati ya mataifa haya mawili zimekuwa zikiongezeka kwa miaka miwili iliyopita, ingawa utawala wa Bush na Obama walikuwa ni mashabiki huru wa serikali ya Beijing; walikuwa wanafurahia kampuni za Amerika kushirikiana na China na kufanya maingiliano katika usambazaji, lakini walifahamu kwamba huku China ikijikita zaidi katika Biashara na Ujasiriamali, Serikali za Amerika na China zinatofautiana pakubwa juu ya demokrasia na haki za binadamu. Donald Trump hafurahishwi na rekodi ya nchi katika mambo hayo mawili. Lengo lake ni “kuifanya Amerika kuwa ukubwa tena” na kurudisha upatikanaji wa kazi katika sehemu yake. Alienda sambamba na Beijing katika biashara.

Ana nukta halali haswa ikiwa nguvu zake zitazingatiwa, katika kufungua masoko ya uwekezaji, vikwazo dhidi ya miradi inayomilikiwa na China na kuzuia wizi wa mali za kitaaluma. Kulikuwepo na majadiliano ya kibiashara, na hatua ya kwanza ya makubaliano ilikuwa imefikiwa. Pamoja na hayo, kulikuwepo na uhasama kuhusu Huawei na hofu kwamba China ingeliichunguza Amerika na washirika wake kama wangeruhusu vifaa vya Huawei kuingia katika miundombinu ya 5G. Kisha janga la virusi vya Korona likaibua hali ya sintofahamu pale ambapo Washington ilipoishutumu Beijing kwa kushindwa kuchukua hatua makini na za haraka dhidi ya Virusi, hivyo kuruhusu kusambaa ulimwenguni.

Sheria mpya ya ulinzi ya China kwa Hong Kong imeibua makubwa  zaidi. Imechukua nafasi na kuipindua katiba ya  Hong  Kong, Sheria Msingi, imedhibiti uhuru wa kiraia wa watu wa Hong Kong, na kupelekea  “nchi moja, serikali mbili” muundo ambao ulitakiwa kubakia hadi 2047 chini ya vifungu vya Azimio baina ya China na Uingereza la mwaka1984. China imepiga hatua ya haraka katika uchumi na katika ushawishi wa kieneo na kisiasa. Mataifa ya Magharibi yanajiuliza ni kwa namna gani dola trilioni moja na ujenzi wa kimiundombinu umewezesha China kufikia hatua hiyo. Haikuwezekana hadi pale Sri Lanka ilipolazimishwa kuachia bandari yake ya Hambantota kwa China ambayo imekuwa ikimiliki makampuni ya bandarini kwa miaka 99 ili kufidia deni ambalo lingewafanya Wamagharibi katika kufahamu mtazamo wa China katika upanuzi wa siasa za kimaeneo. Majirani wengi wa China kutoka kusini mashariki mwa Asia wanaendelea kuzingatia kuongezeka na kupanuka kijeshi kwa China, haswa katika bahari ya China Kusini. Bajeti ya ulinzi ya China imezidi zaidi hadi kwenda sambamba na uchumi wake kufikia; dola bilioni 178 kwa mwaka 2020 ikiwa ni ya pili duniani, na kuongezeka zaidi kwa asilimia 6.6 kutoka 2019 hadi 2020. Utofauti wa China na Amerika hivyo basi ni wa kimfumo, kiuchumi na pia unaongezeka kuwa wa kijeshi. Washington huenda ikawa na sababu zake za kuikaba koo Beijing, lakini kwa miaka mitatu iliyopita Amerika imejitoa katika mashirikiano ya kimikataba mfano ni mkataba wa Paris  kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa na Shirika la Afya Duniani. China imejifunga katika kuyasaidia mashirika haya, ikionyesha mbele ya macho ya wengi kudumisha utekelezaji wa agizo la urafiki na ushirikiano wa kilimwengu. Tunarudi tulipoanzia: Ukuaji wa China wa kiuchumi na ushawishi wa kisiasa na kieneo umeenda sambamba na mpango wa Amerika wa kujitoa katika mpangilio wa kiulimwengu ya baada ya mwaka 1945, mpangilio iliogemea katika ushirikiano wa kimataifa. Ni wazi kwamba hilo litapelekea msuguano mkubwa. Hata ikiwa Donald Trump atashindwa katika uchaguzi wa mwezi 11, tusitarajie kwamba mambo yatarudi kati hali iliokuwepo kabla. Dunia na Amerika zimesonga mbele. Wanaoipinga China wamegawanyika katika pande zote za kisiasa nchini Amerika, huku mgombea wa chama cha Democrat Joe Biden akigombea na Trump katika shauku yake kwa Beijing. [Chanzo: Arab News]

Hali ya sintofahamu kati ya China na Amerika haitapungua na upo uwezekano ikapelekea katika mapigano. Vyovyote vile, swali msingi sio nchi za Kiislamu zitachagua upande upi; bali ni je, nchi za Kiislamu zitaungana na kutumia fursa ya ugomvi huu. Pindi Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alipoasisi dola ya kwanza ya Kiislamu mjini Madina, alikuwa makini na akifuatilia kwa ukaribu mzozo kati ya dola ya Uajemi  na Roma. leo, je ni mwerevu gani katika vikosi vya kijeshi anayeweza kuitumia fursa hii kati ya China na Amerika kisha akaisimamisha tena Khilafah Rashidah kwa njia ya Utume na kuunganisha ulimwengu wa Kiislamu.

Pakistan Yatoa Onyo la Mwisho kwa TikTok juu ya Maudhui Machafu

Waangalizi wa idara ya mawasiliano ya Pakistan wametoa rasmi "Onyo la mwisho" kupitia video fupi iliyotumwa katika mfumo wa mtandao wa TikTok siku ya Jumatatu juu ya maudhui ya wazi yaliyotumwa katika mtandao, wakati ambao mtandao wa moja kwa moja wa Bigo ulifungwa kwa sababu hiyo hiyo.

TikTok, inayomilikiwa na China, imekutana na changamoto nyingi dunia nzima - ikiwa ni pamoja na Australia, India na Amerika - kuhusiana na mambo ya ulinzi na utunzaji wa siri za mtu binafsi. Mamlaka ya mawasiliano ya Pakistan (PTA) ilisema imetuma ujumbe kwenda kwenye mitandano ya TikTok na Bigo kuboresha maudhui yao baada ya kupokea malalamiko, lakini majibu hayaridhishi. "PTA imeamua kuifungia Bigo na kutoa onyo la mwisho kwa TikTok kujitahidi kwa kutumia njia yoyote kuondoa maudhui yasiokubalika, na uozo wa maadili kupitia katika mtandao wake wa kijamii," ilisema. Katika barua pepe iliyotumwa kwenda kwa shirika la Reuters, TikTok ilisema imekusudia kuzidisha mazungumzo na mamlaka hizo katika kuonyesha sera na namna ilivyojizatiti katika usalama wa watumiaji". TikTok ilisema imefuta zaidi ya video milioni 3.7 "zenye kukiuka usalama wa watumiaji" kutoka Pakistan katika nusu ya pili ya mwaka 2019: zaidi ya asilimia 98 zilifutwa kabla ya watumiaji kutoa taarifa na zaidi ya asilimia 89 kabla hawazijatazamwa. Singapore inayomiliki mtandao wa BIGO, haikujibu chochote mara tu ilipo ombwa kutoa maoni. [Chanzo: US News]

Ukweli ni kwamba Pakistan haijachukua hatua yoyote dhidi ya Facebook, YouTube na mitandao mingine kutoka Amerika kwa kusambaza maudhui machafu na ya matusi na hilo linaweka wazi kwamba  Islamabad inailenga  TikTok ili kuiridhisha Amerika badala ya kuchua msimamo mkali kuondoa na maudhui ya matasi kupeperushwa nchini Pakistan.

Ufaransa Yaungana na Amerika, Uingereza katika Kuishutumu China kwa Mateso ya Waislamu wa Uighur

Ufaransa imeungana na Amerika na Uingereza kuikashifu China kwa kuwafunga jela Waislamu wa jamii ya watu wachache katika eneo la Xinjiang. Ufaransa imeyaita mateso hayo ya Waislamu wa Uighur kuwa ni “jambo lisilokubalika” na kuitaka Beijing iruhusu waangalizi huru wa haki za binadamu kuzuru eneo hilo. Waziri wa Mambo ya Kigeni Jean-Yves Le Drian amesema nchi yake inataka waangalizi uhuru wa kimataifa, ikiwa ni pamoja na Balozi wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu Michelle Bachelet waruhusiwe “waingie kwa uhuru” katika eneo hilo. “Vitendo hivyo vinavyofanywa katika eneo hilo havikubaliki kwa kuwa vinakwenda kinyume na makubaliano ya ulimwengu kuhusu haki za binadamu na tunapinga hilo kwa nguvu zote,” alisema, aliongezea kwamba Paris ipo makini na inafuatilia hali inavyo endelea. Serikali ya Uingereza iliambiwa “ichukue hatua kali” dhidi ya China mnamo siku Jumanne kuhusu “mauaji ya kimbari ya Waislamu wa jamii ya Uighur,” na halaiki ya Baraza la Waislamu la Uingereza, mwavuli mkubwa zaidi wa Waislamu wa nchini humo.

Idara ya biashara ya Amerika ilipiga marufuku mashirika 11 ya China kuingia Amerika siku ya Jumatatu kwa kushiriki kwao katika uvunjifu wa haki za kibinadamu dhidi ya jamii ya wachache ya Uighur katika eneo la Xinjiang. Katika mahojiano na BBC, balozi wa China nchini Uingereza Liu Xiaoming mnamo Jumapili alikana kuenea kwa unyanyasaji dhidi ya jamii ya Uighur baada ya video kupeperushwa katika mitandao ya kijamii ikiibua tuhuma za mauaji ya halaiki. Mkoa wa Xinjiang ni nyumbani kwa watu milioni 10 wa jamii ya Uighur. Kundi la Waislamu la Turkic, linajumuisha takriban idadi ya asilimia 45 ya watu wa Xinjiang, kwa muda mrefu limekuwa likizishutumu mamlaka za China dhidi ya ubaguzi wa kiutamaduni, kidini na kiuchumi. Hadi kufikia watu milioni moja, au asilimia 7 ya idadi ya Waislamu wa Xinjiang, wameweka kizuizini katika mtandao mpana wa kambi za “uelimisha upya wa kisiasa”, kwa mujibu wa maafisa wa Amerika na wataalamu wa Umoja wa Mataifa. [Chanzo: The Eurasia Times]

Waislamu wa Uighur kwa mara nyingine tena wamekuwa ni chombo kinachotumiwa na Mataifa ya Kimagharibi dhidi ya China. Wamagharibi wanawatumia tu Waislamu ili kuendeleza malengo yao ya kisiasa na kadhi ya Uighur haina tofauti. Lau ulimwengu wa Kiislamu ungekuwa umeungana na kushikamana chini ya uongozi wa Khilafah Waislamu wa Uighur wangekuwa wanaishi chini ya Uislamu wakilindwa dhidi ya China pamoja na Amerika.

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.