Alhamisi, 18 Ramadan 1445 | 2024/03/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hakuna Haki Ndani ya Nidhamu Dhalimu ya Demokrasia

Habari:
Mnamo tarehe 1 Septemba 2017, mahakama ya juu ya Kenya ikiongozwa na jaji mkuu David Maraga akiwa na jopo la majaji sita walitoa uamuzi uliopelekea kufutiliwa mbali kwa matokeo ya kura za uraisi na hivyo basi kupelekea kubatilisha kutangazwa kwa Uhuru Kenyatta kama raisi mteule. Kati ya majaji sita, wanne walisema kuwa baada ya kuzingatia ushahidi kwa uamuzi wa walio wengi: kifungu 10, 38, 81 na 86 vya katiba na sehemu ya 39(1), 44 (a) na 83 za sheria ya uchaguzi, mtuhumiwa wa kwanza (tume ya IEBC) alifeli, alipuuza na alikataa kusimamia uchaguzi kwa njia na maelekezo ya katiba. Hukumu hii iliitaka tume ya IEBC kufanya uchaguzi mpya ndani ya siku 60. Raila Odinga alisema kuwa haki imetendeka na uamuzi huu ni kielelezo kwa Afrika.

Maoni:

Uamuzi huu wa mahakama ni njama nyengineyo ya walinganizi wa demokrasia kuiokoa nidhamu ya kidemokrasia kutokana na kuporomoka kwake, ambayo tangu 2007 imefeli kutambua 'uwezo' wa watu kupitia kura. Walifanya kampeni za kiwango kikubwa kwa kutumia kila aina ya khiyana kuhakikisha kuwa mabadiliko watakayo leta ni ya kisanii kwa jina la 'demokrasia komavu'; kubuniwa kwa cheo cha Waziri Mkuu kwa Raila Odinga na hatimaye kuapishwa kwake mnamo Aprili 2008 ili kumuwezesha kufikia uongozi kwa niaba ya Amerika. Wakaamsha hekaya ya ICC mnamo 2009 kutoa sura ya kujitolea kwa jamii ya kimataifa katika kujali amani na kumakinisha demokrasia nchini Kenya; na kupitishwa kwa katiba mpya ya 2010 kutoa fursa ya kutatua changamoto za kikatiba zilizo shuhudiwa katika katiba ya zamani.

Haya ni baadhi tu ya mabadiliko hadaifu waliyo yafanyia kazi, lakini kwa kuwa demokrasia yenyewe kama nidhamu ya utawala imechukuliwa kutoka katika mfumo batili wa kirasilimali. Mfumo batili ulio chipuza kutokana na akili finyo za watu lengo lake likiwa ni kutenganisha dini na maisha; hivyo basi hainge tarajiwa kutoa suluhisho ya kikweli kwa masuala yanayo wakumba wanadamu nchini Kenya na ulimwengu kwa jumla. Kwa kuwa mabadiliko hayo yalitokana na msingi wa fikra ya maslahi inayolenga kumnufaisha mteja mkuu. Zaidi ya hayo, hukumu hii inathibitisha yafuatayo:

1. Uhuru wa tume ya uchaguzi ya Kenya IEBC unatiliwa shaka ikiwa inashindwa na hata kuiweka mitambo yake humu nchini na badala yake kuamua kuiweka katika eneo la bwana wake wa kikoloni (Ulaya)!

2. Dori ya waangalizi wa uchaguzi ni kufuatilia uchaguzi huku wakiwa tayari wamejenga fikra ya matokeo yake na hatimaye kutoa ripoti za kumpendelea bwana wao anaye walipa kama ilivyo jitokeza kwa waangalizi wa uchaguzi kutoka Jumuia ya Nchi za Madola, Umoja wa Ulaya, IGAD walio muunga mkono kibaraka wa Uingereza Uhuru Kenyatta huku wale wa taasisi ya Carter Center wakimuunga mkono kibaraka wa Amerika Raila Odinga. Haya yamedhihirishwa kutokana na wengi wao kuuidhinisha uchaguzi huu kuwa wa sawa isipokuwa taasisi ya Carter Center, iliyo sema katika taarifa yake ya mnamo Agosti 10 kuhusu uchaguzi, iliungama kuwa "siku ya uchaguzi mipangilio ya upigaji na kuhesabu kura ilikuwa shwari lakini uwasilishaji matokeo kupitia njia ya kielektroniki haukuwa wa kuaminika."

3. Makampuni ya kimataifa yanajali sana uchumi wao kiasi kwamba walishughulishwa sana na hali ya utulivu nchini Kenya dhidi ya wito wa uchaguzi wa haki na hatimaye kutoa pongezi kwa Uhuru Kenyatta kwa kuchaguliwa tena licha ya kuwepo na tetesi za kutoridhika zilizotoka upande wa upinzani uliodai kuwa kulikuwepo na dosari za wazi katika uchaguzi huo.

Kupatikana kwa mabadiliko ya kweli ni kwa kupitia tu kubeba na kulingania mfumo badala pekee, unaotoka kwa Muumba wa wanadamu Anaye yajua maslahi yao. Mfumo huo ni Uislamu na kutawalishwa kwake ni hakikisho la kweli kwa amani, utulivu na mafanikio. 

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Ali Nassoro

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumamosi, 27 Juni 2020 15:18

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu