Ijumaa, 19 Ramadan 1445 | 2024/03/29
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 IMF Yausakama Uchumi wa Pakistan

(Imetafsiriwa)

Habari:

Waziri Mkuu Imran Khan mnamo Jumatano alihutubia taifa kutangaza kifurushi cha kupunguza hali ngumu ya umma ulioathiriwa na mfumko wa bei. (https://www.dawn.com/news/1655727)

Maoni:

Maafisa wa fedha wa Pakistan wanaofadhiliwa na IMF walikuweko jijini Washington katika wiki za hivi karibuni wakiomba kufunga mkataba na Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) ili kuachilia mgawo uliozuiliwa wa dolari bilioni 1 kutoka kwa kifurushi cha uokoaji, ambacho Islamabad inasema unauhitajika kiasi ili kulinda uchumi wa nchi hiyo unaotapatapa. Mnamo Julai 3 2019, Mfuko wa Fedha wa Kimataifa uliidhinisha kifurushi cha uokoaji cha dolari bilioni 6 kusaidia "kurudisha ukuaji endelevu" kwa uchumi wa Pakistan. Katika muda wote wa mkataba huo uliochukua muda wa miezi 39, IMF itahakiki maendeleo ya Pakistan kila robo mwaka. Kama sehemu ya makubaliano hayo, dolari bilioni moja zimetolewa kwa Pakistan.

IMF imeitaka Pakistan kulipa deni la nje la dolari bilioni 37.359 ndani ya muda wa mpango wa uokoaji wa IMF. Ongezeko la ushuru linalohitajika na IMF lilionekana katika bajeti ya kifedha ya mwaka wa fedha wa 2019, huku serikali ikiongeza lengo la ukusanyaji wa ushuru wa Bodi ya Shirikisho la Mapato (FBR) kutoka rupia trilioni 3.94 za Pakistan (dolari bilioni 25) hadi rupia trilioni 5.5. Tangu mpango wa uokozi, rupia trilioni 1.5 za ziada na ongezeko la trilioni 1.31 katika ukusanyaji wa mapato zinaweza kushuhudiwa.

Mnamo Januari 2020, IMF ilisimamisha mpango huo baada ya serikali kutokubali kuongeza bei ya umeme na kutoza ushuru wa ziada. Ripoti za hivi majuzi za vyombo vya habari zilidai kuwa IMF inadai nyongeza ya Rs4.95 kwa kila uniti ya ushuru wa umeme na kuitaka serikali kutoza ushuru wa thamani ya rupia bilioni 150. Katika mkutano na waandishi wa habari mjini Washington, Shaukat Tarin alikiri kwamba "IMF ilipendekeza kuongeza bei ya umeme na gesi na viwango vya kodi." IMF imetaka hatua zaidi za kuongeza ushuru wa mapato, ushuru wa mauzo, na ukusanyaji wa ushuru wa udhibiti na ikaihimiza Bodi ya Shirikisho.

Kuegemea kwa Serikali ya Pakistan kwenye kifurushi cha uokoaji kumeiweka sera yetu ya kiuchumi mikononi mwa IMF. Pakistan sasa inalazimishwa chini ya sheria kali za ushuru kuongeza ulipaji wa deni la Pakistan. Kwa hivyo mafuta ya kupikia sasa yanafikia zaidi ya 300Rs kwa lita ongezeko la bei kama hilo ambalo halijapatapo kushuhudiwa pia linaweza kuonekana katika bidhaa nyingine msingi kama vile sukari, unga, nyama, maziwa, dengu pamoja na bei ya petroli ikifikia juu sasa kwa karibu 148Rs kwa lita, ongezeko la daima la uniti ya umeme linasababisha matatizo kwa maisha ya asilimia 95 ya watu wanaoishi nchini Pakistan. Pamoja na ongezeko la kodi na bei ya juu ya nishati, Wapakistani pia wanakabiliwa na mfumko wa bei, huku nguvu ya ununuzi ya Rupia ikipungua. Hivi majuzi mfumko wa bei wa Pakistan ulifikia asilimia 9. Na ni wazi kama muanga wa mchana kuwa mfumko wa bei utaongezeka zaidi. Baada ya kusema kuwa IMF sio mkosaji pekee kwani mnafiki Khan anayetumia neno Madina ki Riyasat kila uchao hajitayarishi kuiweka mbali nidhamu yetu ya kiuchumi kutokana na sarafu iso thamani halisi na kutumia nidhamu ya sarafu mbili (dhahabu na fedha) kama ilivyotabikishwa na Mtume wetu kipenzi (saw) mjini Madina.

Mfumko huu wa bei wenye maafa unaweza tu kutatuliwa kwa kutabikisha mfumo ulioteremshwa kutoka mbinguni ambao MWENYEZI MUNGU (swt) ametupa sisi yaani Khilafah. Khilafah itasitisha ulipaji wa riba wa rupia bilioni 300 kwa mwaka na pesa hizi zitatumika kwa mambo ya watu. Dola itawekeza kwenye viwanda vizito, mawasiliano ya simu, nishati na sekta ya madini na sio tu kukomesha ubinafsishaji zaidi lakini pia kurudisha chochote ambacho tayari kimebinafsishwa na watawala vabaraka kabla ya Khilafah. Dola itatabikisha mara moja sarafu ya mbili (dhahabu na fedha) ambazo zitamaliza mfumko wa bei wa kutisha ambao umelemaza migongo ya asilimia 95 ya watu wanaoishi nchini Pakistan chini ya mfumo huu dhalimu wa kidemokrasia wa kirasilimali. Khilafah itaondoa mauzo yote, mapato na kodi nyingine zote za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja ambazo zitampa afueni mara moja kila mtu katika nyanja zote za maisha.

Sasa ikiwa bado tunangoja kitu kitokee kwa faida yetu basi tutaishia tu kwenye kina kirefu cha matatizo hadi tujaribu kusimamisha tena Khilafah na kuwasukuma na kuwahesabu vikali watu wanaomiliki nguvu kuunga mkono mabadiliko ya kusimamisha tena Khilafah.

إِنَّ اللَّهَ لاَ يُغَيِّرُ مَا بِقَوْمٍ حَتَّى يُغَيِّرُوا مَا بِأَنفُسِهِمْ﴿

“Hakika Mwenyezi Mungu habadili yaliyoko kwa watu mpaka wabadili wao yaliyomo naf- sini mwao.” [Ar Raad: 11]

 Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Mohammad Adel

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu