Logo
Chapisha ukurasa huu

بسم الله الرحمن الرحيم

Ardhi Iliyobarikiwa - Palestina: Hizb ut Tahrir Yatoa Wito kwa Majeshi Kusonga Kujibu Uamuzi wa Uvamizi wa Kuwaruhusu Mayahudi Kufanya Ibada zao ndani ya Msikiti wa Al-Aqsa Uliobarikiwa


Jumamosi, 9 Oktoba 2021, Hizb ut Tahrir katika Ardhi Iliyobarikiwa - Palestina iliandaa visimamo vitatu mjini Ramallah, Hebron na Tulkarm, ambapo ilitoa wito kusonga kwa uhalisi kwa majeshi ya Waislamu kujibu uamuzi wa uvamizi wa kuwaruhusu Wayahudi kutekeleza ibada zao katika makawanda ya Msikiti wa Aqsa Uliobarikiwa.

Katika hotuba zilizotolewa na wanachama wa Afisi ya Habari na wanachama wake, Hizb ilisisitiza kwamba kile ambacho Msikiti wa Al-Aqsa unakabiliwa nacho ni jaribio kubwa na shambulizi kali na baya la umbile la Kiyahudi la kulazimisha matambiko yao ya kibiblia katika Msikiti wa Al-Aqsa kwa maandalizi ya kuanzishwa kwa lile linalodaiwa ni hekalu lao katika eneo zima la Msikiti wa Al-Aqsa.

Hizb ilizingatia kuwa uamuzi huo wa mahakama ya uvamizi unasadifiana na maadhimisho ya ukombozi wa Al-Aqsa kutokana na uovu wa Wanajeshi wa Msalaba katika pambano dhahiri kwa Umma wa Kiislamu, na kwamba uamuzi huu usingechukuliwa na Mayahudi na kukidhalilisha Qiblah cha kwanza cha Waislamu lau kama si khiyana ya wasaliti na njama za watawala wahalifu.

- Sehemu ya Kisimamo cha Mjini wa Khalil ar-Rahman (Hebron) -

- Sehemu ya Kisimamo cha Mjini wa Tulkarm -

- Sehemu ya Kisimamo cha Mjini wa Ramallah -

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.